Natafuta mwekezaji kwenye biashara ya vifaa vya ujenzi karakana ya mageti Mapinga Bagamoyo

Natafuta mwekezaji kwenye biashara ya vifaa vya ujenzi karakana ya mageti Mapinga Bagamoyo

manlike lucho

New Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
2
Reaction score
4
Habari wana jukwaa na wawekezaji wote. Mimi ni mjasiriamali mwenye uzoefu wa miaka minne katika sekta ya ujenzi hapa Mapinga Bagamoyo.

Eneo hili lina kasi kubwa ya ujenzi wa makazi kwa sasa.Mradi wangu unaunganisha vifaa vya ujenzi yaani hardware pamoja na karakana ya kutengeneza mageti na vyuma.

Tayari nina rasilimali na mali zilizopo za thamani ya shilingi milioni kumi na tano ambazo ni pamoja na kiwanja cha biashara, mashine ya kufyetulia tofali, na mzigo wa duka uliopo sasa wa thamani ya milioni tano.

Natafuta mwekezaji wa kuongeza mtaji wa shilingi milioni kumi na tano ili kupanua duka letu la hardware na kununua vifaa vya kisasa vya karakana.

Ofa yangu: Mwekezaji atapata gawio la laki mbili kila mwezi kwa miezi sitini. Pia mtaji wake unalindwa kisheria kwa asilimia mia moja na rasilimali zilizopo sasa hivi.

Mwishoni mwa miaka mitano atalipwa mtaji wake wote wa milioni kumi na tano kwa mkupuo mmoja.

Kama umevutiwa na ofa hii na ungependa tuonane ana kwa ana hapa Mapinga au Dar es Salaam ili kukagua mradi na kuona andiko kamili la biashara, tafadhali nitumie ujumbe wa faragha yaani PM hapa jukwaani ili nikupe namba zangu za simu na tuchat.
 
Natamani kujua, majukumu ya muwekezaji yapoje,
Na nikuwekeza pesa tuu afu mtuu anakaa pembeni au anatakiwa kuw sehemu yauendeshaji wa iyo biashara
 
Natamani kujua, majukumu ya muwekezaji yapoje,
Na nikuwekeza pesa tuu afu mtuu anakaa pembeni au anatakiwa kuw sehemu yauendeshaji

Natamani kujua, majukumu ya muwekezaji yapoje,
Na nikuwekeza pesa tuu afu mtuu anakaa pembeni au anatakiwa kuw sehemu yauendeshaji wa iyo biashara
Shukran bwana blondy. Mwekezaji hana jukumu lolote katka uendeshaj wa biashara lakn anayo nafasi ya kufuatilia na kujua mwenendo mzma wa biashara
 
Back
Top Bottom