Natafuta mwenza

Natafuta mwenza

SAINT MATATA

Member
Joined
Dec 5, 2022
Posts
21
Reaction score
34
Ni mara ya kwanza nakuja jukwaani hapa kutafuta mwenza. Litakuwa jambo jema kama nitampata mwenye kunififkiria na kuruhusu tuishi pamoja.

Kabla ya kuweka vigezo, naomba nieleze machache hapa chini:
Sijafanikiwa kuwa na kazi maalum ya kuniingizia kipato, kwa hiyo sina kazi kwa sasa japo nimesoma kwa level ya chuo kikuu.

Wasifu wangu;
1. Umri wangu ni miaka 35+.
2. Si mrefu wala mfupi sana.
3. Nina mtoto mmoja.

Mwanamke atakaenifikiria;
1. Awe mrefu wastani.
2. Akubali kuishi na mimi kwa sasa nikiwa naendelea kujitafuta ili kukaa sawa kimaisha.
3. Kabila lolote.
4. Mkristo.

Karibu Pm
 
Hivyo vigezo vyako vingekubeba zaidi ungekuwa jinsia ya KE. Ila kwa jinsia yako na vigezo hivyo nakutakia kila la heri.

Wanawake huwa na roho mbaya sana ya kutotaka mategemezi. Mwanamke akiwa kapuku anatarajia wanaume wamuangalie na kumtunza ila hawatarajii kutunza wala kuangalia mwnaume kapuku.
 
Nashukuru kwa maoni mdau. Ngoja niendelee kusubiria huenda akajitokeza mmoja.
 
Ni jambo jema ndg. Hongera Sana Kwa kuthubutu. Mkristu wa dhehebu Gani?. Niko na nia njema kabisa kukuuliza hivi.
 
Back
Top Bottom