Natafuta mwenza

Natafuta mwenza

Habari ya wakati huu. Nimeleta mrejesho kwa kipindi ambacho nimekuwa na uhitaji wa mwenza na nikaposti humu. Lakini waliokuja pm ni wababa waume za watu na wengine wanakuja for funny tu, wakihisi hii ni sehemu ya kula kucheza na kuondoka.

Wakati Niko seriously katika Jambo hili na Nina uhitaji wa mwenza, ili kama tukija kuelewana vizuri basi tuweze kufunga pingu za maisha. Haimaanishi kuja hapa kuwa eti mtaani hawapo au kanisani hawapo, hapana. Bali Kuna sababu zilizosababisha nikaja kwenye platform hii.

Bado sijachoka, ninauhitaji wa mwenza , awe na age kuanzia 32 mpaka 40. Awe mkristo ikiwa mkatoliki itapendeza zaidi, awe mkoa wowote, akiwa na watoto sawa, ilmradi tu ajue majukumu yake kama baba wa familia. Awe na kitu kinachomuingizia kipato ili tu tusilale na njaa.

Sifa zangu ni mkristo katoliki, nimejiajiri, nna watoto 2, miaka yangu 32, mwembamba. Naishi dsm.
NOTE:.

ANAYEKUJA UHAKIKISHE SIYO MUME WA MTU NA PIA UKO SERIOUSLY UNAHITAJI SAFARI YA MAHUSIANO. OTHERWISE SIHITAJI KUKUONA PM.

KARIBU PM KAMA UNA SIFA , UNAHITAJI MTU MWENYE SIFA KAMA ZANGU, NA UNA NIA THABITI YA MAHUSIANO.

SIO KWASABABU UMEONA NI SINGLE MOTHER BASI UKAHISI NI SEHEMU YA KULA KIRAHISI NA KUONDOKA. BE CAREFUL.
Mtoa mada vipi hukunionea ERoni huko? Maana kapotea haonekani nyumbani.
 
Kila la heri mkuu... sema ukisoma comment nyingi humu wengi wanatamani kujua zaidi kati yako wewe na mzazi mwenzio status inasomaje.

So ushauri wangu kwa any woman ambae ako na mtoto/watoto na anahitaji mwenza humu ajitahidi kuelezea kwa kina hapo kwenye connection kati ya yeye watoto na baba yao ipo vipi vipi yani.

Kitu ambacho wanawake wengi ambao mmezalishwa na kuachwa hamjui au mnajua ila hamna uhakika ni kwamba wanaume ambao wamewazalisha hata kama wameoa huwa wanafurahia sana kuwaona mkiwa hamjaolewa coz walio wengi wako na wivu na nyie bado (hii ni asili ya Kila mwanaume) kwahiyo once akijua unaishi na mtu lazima ataanza kutekenya tekenya na ukishtuka tu anaweka na hapo ndipo atakapojionea fahari na nguvu ya uwanaume wake.

Kwahiyo inawezekana wewe sasa hivi umemove on na jamaa aliyekuzalisha unamuona hana time na wewe like amemove on ni kwasababu anakuona ukosingle na ukiingia kwenye mahusiano ndio utajua uhalisia wa kwamba kweli amemove on or bado.

Na mliowengi kwenye hili eneo ndio huwa mnafeli ingawa kwa mwanzoni huwa mnajitahidigi sana kuruka viunzi ila baada ya kulizoea penzi jipya na kumuona jamaa mpya aliyekuheshimisha wa kawaida unaanza kumithirisha mambo na hatimae mdogo mdogo unaanza kumpa attention mzazi mwenzio na sisi wanaume target yetu huwa ni moja tu ingawa tunaweza kuweka uongo mwingi ili muamini kwamba hatuko huko ila ukijaa tu ni shwaaaaaaaa 😆😆😆😆.

WEKA DETAILS ZA BABA WATOTO WAKO ILI TUJUE TUKIJA INBOX TUJE TUKIWA TUMEJIRIDHISHA.
 
Back
Top Bottom