Tafta gereji nzuri omba kujitolea upate uzoefu.
Naamini magari mliyoyasomea NIT ni yale ya kuzamani, mifumo ya kizamani. Magari ya sasa mwngi ni ya mifumo mipya na ya kisasa, rahisi kutengeneza hasa kwa watu mlioenda shule na ukapata vifaa sahihi. Hivyo mtaani utakutana ma magari yenye mifumo tofauti na uliyosomw NIT.
Sasa wewe una advantage moja, una shule, ila huna uzoefu na ujuzi ila una maarifa hivyo ni rahisi ku-excell kwenye hiyo fani iwapo utakua tayari kujifunza na kufundishwa.
Huko kwenye kujitolea usijifanye msomi, maana utakuta watu waliomaliza darasa la saba ila wana ujuzi, kua tayari wakufundishe, ukiongeza na maarifa yako utakua mzuri zaidi.
Baada ya hapo, utaanzisha gereji yako na kuanza kupiga hela.
Kila la heri bwana mdogo.