Kwa mwenye taarifa ya shirika lolote linalolipa mshahara mzuri au kampuni Mimi nina taaluma mbili 1. ni mwalimu kada niliitumikia kwa muda mrefu na naendelea kufundisha shule za msingi. 2. Mimi ni Counselor nina shahada ya unasihi (Bachelor of couselling). Baada ya kumaliza masomo yangu ya shahada niliomba kubadilishiwa cheo lakini kutokana na ukiritimba wa nchi yetu nikaambiwa shahada yangu haitambulikani licha ya umuhimu wa taaluma hiyo kama nitakavyoeleza umuhimu wake hapa chini. Baada ya hapo nikaomba likizo bila malipo ili nifanye kazi na Kituo cha Afya kama mratibu wa UKIMWI nikakataliwa. Hata hivyo nikaamua kufanya kazi kwa mkataba wa mwaka mmoja kwa muda fulani mwisho wa juma na kila baada ya kazi. Baadaye ya mkataba kwisha niliamua kuachana kutokana na kipato walichokuwa wananilipa. Katika Tanzania nimegundua kuwa ili upate kazi lazima uwe na mtu wa kukupigia debe bila kujali uwezo ulionao. Aidha uwezo wa viongozi wetu ni mdogo kutokana na sifa wanazoajiriwa kutokana na kufahamiana na nani baadala ya kuajiriwa kwa kuwa unajua nini. Nilipowambia nimemaliza shahada yangu nilijibiwa kuwa shahada yangu haitambulikani bila kuuliza nilichosoma kina faida gani katika jamii. UFUATAO NI UMUHIMU WA UNASIHI (COUNSELLING) 1.Ni muhimu katika kutoa elimu ya malezi bora, Tuna mafisadi wengi kwa vile tu wana matatizo ya kisaikolojia kwa vile tu waliikosewa kulelewa kisaikolojia na kujikuta hawajiamini. kwa vile hawajiamini wanafikiri wakiwa na mali basi wataheshimika, wataonekana, kwa ufupi wanatafuta kujulikana na kulindwa na mali. Na ili mtoto ajiamini anatakiwa apate malezi bora kwa kufuata kanuni bora za kimalezi kisaikolojia akiwa na umri wa miaka 0-5 kisha miaka 5-12 Akikosewa hapo basi mtoto huyo hataweza kujiami. Na mtoto anayekosa kujiamini basi ataweza kushiriki katika matendo ya ulevi, umalaya na mambo mengi maovu akiongozwa na wale wenye tabia mbaya kwa kupelekeshwa. Kwa hiyo tabia mbaya kama kuvuta bangi, kuiba, rushwa n k ni matokeo ya jamii kuiga kwa vile tu hawajiamini. Muhimu hapa ni kuwapa nafasi wataalamu watoe elimu jinsi ya kulea watoto ili waweze kujiamini na kuwa na jamii bora. Leo hii waafrika wengi hawajiamini kwa vile tu Wazungu waliwaharibu waafrika wajione hawafai. Ni viongozi wachache katika Afrika wanaoweza kuamini kuwa maendeleo ya waafrika wanaweza kuleta maendeleo yao pasipokutegemea wazungu. Unasihi kwa ngazi ya shule utasaidia wale wanafunzi wasiojiamini waweze kujiamini pale wataalamu wa kisaikolojia (wanasihi ) watakaporejesha kujiamini kwa kuwajenga kisaikolojia waliopoteza kujiamini. Kuwasaidia wale waliopoteza wapendwa wao na kuathirika kisaikolojia, wanaoumwa magonjwa yanayosababisha wanyanyapaliwe. Familia wapate elimu kuhusu umuhimu wa kuvumiliana katika ndoa ili kulinda madhara yatakayowapata watoto endapo wataachana Kutoa elimu kuhusiana na matatizo ya kisaikolojia kama vile athari za msongo wa mawazo nakadhalika. msongo wa mawazo una madhra makubwa katika kila sekta, mfano daktari mwenye msongo wa mawazo anaweza kumpa dozi isiyostahili mgonjwa na kusababisha madhara zaidi ikiwa ni pamoja na vifo. mwalimu anaweza kufundisha au akawa mkali kwa mwanafunzi kwa vile tu anamsongo wa mawazo, Anayefanya viwandani au kushughulika na mashine anaweza kuharibu vifaa au kuweza kupata ajali kwa kujikata na mashine kwa vile tu anamsongo wa mawazo. Hivyo ni vema ofisi ziwe na wanasihi kwa kila sekta ili watu wapate nafasi ya kupata msaada wa kisaikolojia ili kupunguza msongo wa mawazo. Zifuatazo ni baadhi ya dalili za msongo wa mawazo 1.kula sana au kupoteza hamu ya kula 2.kukosa usingizi au kulala usingizi sana 3.kupenda vitu vitamu kama vile pipi, biskuti, soda 4.kunywa pombe sana 5. Kupoteza hamu ya tendo la ndoa au hamu ya tendo la ndoa kuzidi 6. Kupoteza hamu ya kuwasiliana na ndugu au marafi (Kuwachukia) 7. Kujiskia mchovu bila sababu za msingi Hizo ni baadhi tu ya dalili za msongo wa mawazo Ili kupunguza msongo wa mawazo (stress) fanya yafuatayo 1. Fanya mazoezi ya viungo kama kukimbia, kuendesha baiskeli nk 2. Punguza vyakula vya mafuta, kula mboga na matunda kwa wingi 3. Jithidi kuwa jirani na mtu unayempenda au kundi la watu baadala ya kuwa peke yako 4. kama kuna mnasihi jirani unayemfahamu mwombe ushauri 5. Fanya kitu unachokipenda kama vile kuangalia mpira, tv nk 6. Punguza kufanya kazi, uwe na muda wa kupumzika Nimejaribu kuonyesha kwa ufupi umuhimu wa Unasihi katika jamii ya kitanzania Nawasilisha .