Natafuta nafasi ya kuichezea klabu yoyote inayoshiriki NBC Premier League Tanzania

Jo Assistant

Senior Member
Joined
Jun 20, 2014
Posts
195
Reaction score
199
Habari wadau wa Jamii Sports?

Nina ombi moja kwenu.

Mimi ni kijana Mtanzania mwenye kujituma, mwenye nidhamu na mchapakazi. Ninaandika ili kuonyesha nia yangu ya kuomba nafasi ya kuichezea klabu yoyote inayoshiriki Ligi kuu ya NBC, kwa nafasi ya "Mid fielder" au "Defender". Nipo tayari kusajiliwa na klabu yoyote na kuanza kuchezea kikosi chochote.

Nilipokuwa form 3 nilicheza katika timu iliyofanikiwa kutwaa ubingwa katika mashindano ndani ya shule yangu. Wengi walikubali sana kipaji changu hadi baadhi ya wanafunzi wenzangu waliniita freemason kwa kunionea wivu, maana nilikuwa nikicheza kwa umakini, nidhamu na ustadi wa hali ya juu uwanjani.

Bahati mbaya familia na marafiki hawakuniunga mkono tokea hapo awali, hivyo nililazimika kuendelea na masomo. Wote niliowahi kuwashirikisha kuhusu shauku yangu ya kucheza mpira hawakunipa nafasi wala kunisaidia kiuchumi au kulea kipaji changu.

Lakini sijakata tamaa mpaka sasa. Nina ndoto ya siku moja kuichezea klabu mojawapo nchini hadi kutwaa kombe la klabu bingwa Afrika, pamoja na Taifa Stars (timu ya Taifa) hadi kufanikiwa kutinga katika timu zitakazocheza kombe la dunia 2026.

Natumaini kuwa wahusika mtanipokea na kunipa nafasi katika klabu. Pia, natumaini kuwa wenye connection mtazingatia na kuni'recommend kwa wahusika. Nami nitakubali kuwa chini kufundishwa, kuelekezwa na kushirikiana vizuri na wachezaji wenzangu ili kipaji changu kiweze kukua zaidi, nami niweze kucheza na kufanikisha malengo ya klabu.

Ahsanteni sana wakuu kwa kuzingatia.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unachotakiwa ni kujaribu tu bahati yako kwa kujitolea kufanya majaribio kwenye zile timu zinazotangaza kutafuta wachezaji wa ligi kuu! Mfano Mtibwa fc, nk

Hakuna njia ya mkato kijana wangu. Maana kuna wenzako wengi tu wako mtaani, huku wakiwa na uwezo mkubwa kuliko wewe, lakini hawajapata nafasi ya kucheza ligi kuu.
 
Sawa mkuu. Nimekupata vizuri. Majukumu kadhaa yamekuwa yakinibana kwa muda mrefu, ila nitajitahidi nitumie nafasi nitakazozipata.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una miaka mingapi?
Una kitambulisha au namba za nida?
Height yako na uzito wako?
Elimu yako?
Na unapatikana mkoa gani?
Video clip hata ya dakika 5 itapendeza zaidi.
Miaka: 26
Kitambulisho cha NIDA: Ndiyo ninacho
Height: 163cm
Elimu: Degree
Mkoa ninaoishi: Kigoma (ila naweza kuondoka hivi karibuni na kwenda Dar es Salaam)

Mkuu hapo kwenye 'Clip' mpaka nijipange (uchumi umenikwamisha sana kwenye vitendea kazi).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah, Interview Za Soka Mkuu huwa Hazina 'short cut' .

Kipaji huwa kinaonekana Uwanjani..! Kote huko hawajakuona mpaka uje huku..!

Popote Ulipo jitahidi kuonyesha kwenye miguu yako Unachokiona nini?

Nina imani hutakuja tena hapa jukwaani,Bali Sisi ndo tutakuwa tunajikomba kwako..!

Hivi Yule Chama unavyomuona anahitaji promo..?
 
Kama upo kigoma nenda JKT kanembwa kafanye majaribio mkuu huwezi jua maana hata Jamie Vardy alianzia madaraja ya chini kabisa.
 
Nakubaliana na wewe asilimia 100% kabisa.

Ni kweli sikuchangamka vya kutosha, lakini ni kwa sababu ya wazazi, ndugu, jamaa na watu wangu wa karibu ambao walisababisha nikose muda na nafasi ya kujichanganya uwanjani. Itabidi nitafute wadau na watu wengine watakaonielewa na kuniunga mkono. Bado naendelea kufanya survey na kufuatilia fursa huku Kigoma nilipo. Mambo yakikaa vizuri, naamini nitaonekana tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ingekua Morogoro au Dar ingekua rahisi kidogo ila fanya mtu akurekodi video clip ukiwa mazoezini au mechi Ili watu waone uwezo wako.
 
Duu miaka 26 muda wote ulikuwa wapi. Mimi na miaka 25. wakati naanza kidato cha 5 2014 nilikutana na David kisu kipa wa namungo tukawa tinasoma nae sidhani kama mmepishana miaka jamaa kwa kipindi kile alikuwa anasifika wilaya nzima kwa udakaji wake.

2015 wakati tunaingia kidato cha 6 jamaa akaacha shule. 2016 mwezi wa kumi na moja wakati nimeanza chuo kulikuwa na gemu ya taifa stars inapigwa nikashangaa kumuona goli kipa wetu ni david kisu nilibaki mdomo wazi.
Baada ya hapo amesha cheza yaani kacheza sana vilabu kadhaa hadi simba leo yuko namungo .
Mpaka sasa hivi sidhani kama anachakupoteza. Mpira ni umri ungekuwa hata na miaka 18 angalau ungepambana miaka 26 kibongo bongo umechelewa
 
Usijali, nimekupata vizuri. Ahsante.

Ni kweli kuwa kwa bongo bado watu wengi tuna "fixed mindsets" katika masuala mengi ikiwemo yale yanayohusiana na mpira. Ndiyo maana tunaona kuwa mambo mengi hayawezekani kulingana na umri, jinsia au mazingira. Lakini, binafsi naamini katika malengo na maono. Hata ikibidi nianze from scratch, sitakata tamaa.

Najua kuwa uhitaji wa wachezaji wazuri nchini bado ni mkubwa na ya kuwa bado wapo watu mbalimbali kila mkoa wanaotafuta wachezaji wazuri. Mimi nitaendelea kutumia kila fursa nitakayopata katika kucheza mpira uwanjani. Niliamua ku'post uzi huu ili kuonyesha nia yangu njema. Yamkini ipo siku nitakutana na hao watu sahihi.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
JF unaingia kwa kutumia kifaa (device) Gani?
 
Kwa umri wako ,katika soka wewe ni mzee umeshachelewa,samaki mkunje angali mbichi,mbwa mzee hafundishiki
 
je unajihusisha na timu za hapo mtaani kwako?.

Kwa kucheza mtaani yaweza kuwa rahisi kuonwa na Mtu/Watu na wakaweza kukunadi kwa Wahusika...na ukinadiwa na Mtu au Watu itakuwa rahisi sana kuitwa kuliko kujinadi mwenyewe.

Ingawa hiyo haiondoi ukweli kwamba kama kipaji unacho unacho tu, wanasema Pembe ya Ng'ombe hajifichiki...jitahidi kujichanganya kila kulipo na Kiwanja wanapocheza mpira ili Wadau wakuone.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…