Jo Assistant
Senior Member
- Jun 20, 2014
- 195
- 199
Habari wadau wa Jamii Sports?
Nina ombi moja kwenu.
Mimi ni kijana Mtanzania mwenye kujituma, mwenye nidhamu na mchapakazi. Ninaandika ili kuonyesha nia yangu ya kuomba nafasi ya kuichezea klabu yoyote inayoshiriki Ligi kuu ya NBC, kwa nafasi ya "Mid fielder" au "Defender". Nipo tayari kusajiliwa na klabu yoyote na kuanza kuchezea kikosi chochote.
Nilipokuwa form 3 nilicheza katika timu iliyofanikiwa kutwaa ubingwa katika mashindano ndani ya shule yangu. Wengi walikubali sana kipaji changu hadi baadhi ya wanafunzi wenzangu waliniita freemason kwa kunionea wivu, maana nilikuwa nikicheza kwa umakini, nidhamu na ustadi wa hali ya juu uwanjani.
Bahati mbaya familia na marafiki hawakuniunga mkono tokea hapo awali, hivyo nililazimika kuendelea na masomo. Wote niliowahi kuwashirikisha kuhusu shauku yangu ya kucheza mpira hawakunipa nafasi wala kunisaidia kiuchumi au kulea kipaji changu.
Lakini sijakata tamaa mpaka sasa. Nina ndoto ya siku moja kuichezea klabu mojawapo nchini hadi kutwaa kombe la klabu bingwa Afrika, pamoja na Taifa Stars (timu ya Taifa) hadi kufanikiwa kutinga katika timu zitakazocheza kombe la dunia 2026.
Natumaini kuwa wahusika mtanipokea na kunipa nafasi katika klabu. Pia, natumaini kuwa wenye connection mtazingatia na kuni'recommend kwa wahusika. Nami nitakubali kuwa chini kufundishwa, kuelekezwa na kushirikiana vizuri na wachezaji wenzangu ili kipaji changu kiweze kukua zaidi, nami niweze kucheza na kufanikisha malengo ya klabu.
Ahsanteni sana wakuu kwa kuzingatia.
Sent using Jamii Forums mobile app