Natafuta/nahitaji mchumba

Natafuta/nahitaji mchumba

Bhudagala

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2014
Posts
325
Reaction score
311
Nina miaka 24 hadi sasa, mpango wangu wa kuoa ni 2018 {NDOA RASMI). Najua sifa za mchumba zipo ambazo hawezi kujipa yeye bali mipango ya Mungu. Nahitaji walau awe na sifa hizi..

1.Urefu wa kuanzia futi 4.5 hadi 5.8.(mimi nina futi 5.8 )

2. Rangi: hapa awe naturally black. (mimi mweus pia)

3. Elimu: awe na elimu kuanzia kidato cha nne(form four) asizidi kidato cha sita (form six). (mimi wakati huo ntakuwa na shahada [degree], kwa sasa niko mwaka wa 3)

4. Kazi. Asipokuwa na kazi hakuna shida, endapo ana kazi basi kazi hiyo iwe inatambulika kijamii na inaendana na utamaduni wa jamii ya kitanzania - iwe kaajiriwa ama kajiajir. (mimi kazi bado sijapata lakini kufikia 2017 ntakuwa ajirani wakati huo nitakuwa naendelea na kaz za kibiashara)
5. Awe na moyo wa kumsaidia mtu yeyote atakayefika kwake(kwetu) kama anafaa kuhudumiwa. Kwa ufupi awe mkarimu. (mimi nina uwezo wa kukaa na mtu yeyote kulingana na mazingira)

6. Na sifa zingne nyingi zinazoweza kumtambulisha kuwa mke wa mtu.

7. Kabila/kanda/mkoa: Matarajio yangu ni kupata mke toka maeneo ya TABORA, SHINYANGA, MWANZA, GEITA NA SIMIYU. (mimi Msukuma wa Mwanza)
NB: UCHUMBA sio tendo la ndoa, naomba ieleweke kuwa nahitaj mke wa maisha sio uchumba wa tendo la ndoa hatimaye kutofikia malengo, bali ni kuwa na mtu ambaye nitakuwa matarajio ya ndoa.

Unaweza kuja DM pako wazi

Hapo hakuna usumbufu maana sifa ninazotaka, nimetaja na mimi jinsi nilivyo, kuna maswali au ungeweza kujua zaid, waweza kunitafuta hapo direct.
 
acha kujidhalilisha kijana na usomi wako..huko chuon hujaona mtu aisee?
 
kuna vitu vinashuka thaman ktk nyakat iz jaman? pia misingi ya ndoa haifutw ndio maana ndio maana ndoa nyng znavunjika.
 
Huo urefu tutapimaje sasa kujua haya lililo chaguo lako litakuja kwa wakti muafaka kua mpole na mvumilivu huku ukimshirikisha Allah katika maamuzi yako
 
Huo urefu tutapimaje sasa kujua haya lililo chaguo lako litakuja kwa wakti muafaka kua mpole na mvumilivu huku ukimshirikisha Allah katika maamuzi yako

Nafikiri kila mtu anajijua kimo chake.....
Asante kwa ushauri
 
Namshukuru Mungu, nilipata mchumba na sasa mambo yako fresh.
 
Back
Top Bottom