Ah! Kumbe Chanika, ambako ukiingia kichwa kichwa utaambiwa ni Chanika kumbe ni Kisarawe! Kama ni viwanja vya aina hiyo Arusha unaweza kuvipata hata kwa 1M. Ni kichekesho kujidanganya eti Arusha viwanja ni ghali kuliko Dar es salaam wakati kasi ya ujenzi kwa Dar ni kubwa maradufu ya Arusha, na demand ya viwanja kwa Dar ni kubwa kuliko Arusha! Mbaya zaidi, wakati Arusha bado kuna maeneo kibao yanayoweza kupimwa viwanja tena wala sio mbali sana na city center, kwa Dar es salaam hayo "maeneo kibao" HAYAPO unless iwe ni more than 30km from the city center!