Akotia
JF-Expert Member
- Dec 16, 2016
- 590
- 1,405
Wadau wa JamiiForums,
Habari za jioni. Ninaomba msaada wenu.
Ninatafuta nyumba ya kupanga yenye vyumba viwili (2 bedrooms) eneo la Mbezi Beach Chini. Bajeti yangu ni kati ya Tsh 500,000 hadi Tsh 600,000 kwa mwezi.
Kinachonifanya niandike hapa ni kwamba kwa sasa hali yangu ya kifedha ni ngumu na sina uwezo wa kulipia gharama za dalali.
Hivyo, ninaomba sana kama kuna mtu yeyote anayemiliki nyumba anayopangisha moja kwa moja (baba au mama mwenye nyumba) au anayemfahamu baba au mama mwenye nyumba mwenye nyumba ya aina hiyo, tafadhali sana niarifu. Nitashukuru sana kama mtanisaidia kuepuka gharama za udalali.
Ninahitaji kupata nyumba hii ifikapo kesho . Najua ni muda mfupi sana, lakini nimejikuta katika hali hii na nina matumaini mema kupitia jukwaa hili.
Tafadhali ni PM (Private Message) au niandikie hapa chini kama una taarifa yoyote.
Asanteni sana kwa ushirikiano wenu na muda wenu.