Natafuta PANYA maana naona PAKA wangu anajinenepea tu. Analala masaa 24

Natafuta PANYA maana naona PAKA wangu anajinenepea tu. Analala masaa 24

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Wadau mimi napenda kufuga hapa kwangu nina Mbwa,Paka, Ng'ombe wa Maziwa na Kuku pia.

Mbwa nmeona kazi yake maana kuna siku kibaka alijichanganya kuruka ukuta kabla sijaweka Fensi ya Umeme... Tulimkuta hoi. Hawa mbwa nikawapenda zaidi.

Kuku tunapata Mayai na Nyama pia. Ng'ombe tunapata maziwa tunashukuru kuna siku tutapata hata nyama. Ila nawaza ingewezekana hata kwa ng'ombe unakata nyama kidogo unakula inaota nyingine ingekuwa bomba sana kuliko kumuua wote.

SHIDA IPO HAPA. Humu ndani hamna panya. So namwona paka ame relax kinyama.... Amekuwa bonge kweli. Hana anachofanya....analala 24x7 yaani huwa ananitia hasira sana. Anakula tu msosi home na kulala anabadili tu sofa na sometimes anaenda ota jua nje.

Ukimtizama mashavu kama mimba ya panya. Mpaka nimepata wazo la kutafuta panya hata wawili niwalete hapa home ili sasa huyu paka ajifunze kudeal nao maana mapaka kama hawa huwa wanakuwa na Ujinga fulani. Huchelewi kumkuta anakula msosi wanashare na panya kwenye sahani moja. Au unaweza kuta kalala na panya kamlalia kifuani.wanakoroma tu.

Ndio nataka nifahamu hili jambo nisije nikawa nafuga paka wa maonesho tu. Nitapata wapi panya? Hilo ndio linalonisumbua.
 
Omba usije pata panya kama Jerry maana huyo paka atachezea sana na familia mtahama muache nyumba
 
Wewe unasema unamlea paka wakati paka anaona anakulea wewe...ukitaka jaribu kumzingua.

Utashangaa anaondoka siku tatu harudi, akirudi anakaa dakika kadhaa anaondoka zake hana time na wewe tena.

Baadae utashangaa anamaliza wiki ama mwezi haionekani, hapo ndio utajua wewe na paka nani anamlea mwenzake.

Kifupi paka hana shida ya kuishi na binadamu, Ila binadamu ndio anashida ya kuishi na paka....
 
ondoa paka urudishe panya, ndipo ulete tena paka.......
ukisema upeleke ndani mwako panya bila ya kumuondoa paka kivyovyote watakimbia kwa khofu ya kuliwa
 
Mkuu huyo paka mpangie majukumu mengine,kaa naye mweleze kabisa ulimnunua kwaajili ya kukamata panya sasa kwakuwa panya hawapo mwambie majukumu unabadili,mwambie hata kuwabembeleza vifaranga vya kuku kuliko kulala tuu masaa 24,au mpangie kazi za njee hata kwenda kuwinda ndege wa poriii mwambie kwawiki unataka ndege wawili...
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Atakuwa paka wa kinondoni ila acha wivu mkuu
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]watu mnaroho za korosho sijawai ona....panya hawapo sababu paka yupo siku muondoe utaona purukushan lake......kuna paka wa mtaani alizalia kwenye compound yangu afu akatelekeza watoto mkee wangu hapendagi paka kiivyoakawa anawafukuza daily ila wanajificha kweny mbao flani ....siku mtoto akaona nyoka ila mpaka aje aseme nyoka alikuwa ashapotea kusiko julikana baada siku tatu tunakutana na nyoka 2 zimeparuliwa hatar plus panya hawaonekani kabisa tukaona hii ni added advantage hatuna habari nao sikuizi ila usikosee usiku ukaacha dirisha wazi utajuta
 
Mkuu huyo paka mpangie majukumu mengine,kaa naye mweleze kabisa ulimnunua kwaajili ya kukamata panya sasa kwakuwa panya hawapo mwambie majukumu unabadili,mwambie hata kuwabembeleza vifaranga vya kuku kuliko kulala tuu masaa 24,au mpangie kazi za njee hata kwenda kuwinda ndege wa poriii mwambie kwawiki unataka ndege wawili...
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] JF kibokooooh lol
 
Back
Top Bottom