Natafuta Partner kwenye kilimo

beko

Senior Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
189
Reaction score
91
Harini wadau wa JF,

Nina shamba ekari 50 zenye rutuba maeneo ya Jaribu Rufiji, mimi sina muda wa kufuatatilia/ au kuendeleza, natafuta mtu mwenye nia, mtaji wangu uwe ni shamba, yeye aendeleze, alafu tutakubaliana namna ya kugawana mapato.

Ardhi hiyo inafaa kwa mazao yafuatayo;

1. Mihogo
2. Mananasi
3. Ufuta
4. Matunda kama vile mapapai, machungwa, na aina zote za mboga mboga.

Unaweza kufanya kilimo cha drip irrigation, ukichima maji yapo mengi tu.

Kwa yoyote anayependa hii fursa anakaribishwa.

Tuma private message
 
Mkuu, hapo umechemka, chakukusaidia kodisha tu eneo lako, nazani ushauri huo unatosha, sizani kama mtu atakubali kugalimika kulima na kuhudumia halafu mtafute mgawo, we kodisha na kila mtu afanye mambo yake.
 
sio ushauri mzuri, tulia wenzako wanataka
 
sio ushauri mzuri, tulia wenzako wanataka
hamna anayetaka. yaani badala mtu anunue shamba huko liwe lake na huko ni cheap, aje akufanyie kazi!. lini tumerudi kwenyee feudalism?
 
beko

umeshapata????? au bado kama bado nijulishe tufanye biashara
 
Last edited by a moderator:
beko

niuzie hilo shamba. haya mambo ya kufanyisha wengine kazi wewe umekaa tu halafu akivuna akugawie yamepitwa na wakati. huo ukabaila tumewaachia wahindi wahindi
.
 
Last edited by a moderator:
beko

mkuu wewe kodisha hilo shamba kwani hakuna mjinga ambae atakubali ujee ugawane nae mazao maeneo hayo bei ya kukodi shamba tena zuri lilo andaliwa tayari kwa kilimo ni 25000/ kwa ekari moja.

Tukisema uchangie na mtu wewe mchango wako ni 1,250,000/= (25000 mara 50) jee upo tayari upewe faida ambao itakwenda sawa na huo mtaji wako ? Mwenzio atatumia zaidi ya 30milioni kwa 50 (60,000/=@1)

hapo mwenzio atakuwa ametumia karibu mara 20 ya mtaji wako jee na wewe upo tayari achukuwe faida mara 20 zaidi yako??? Njia rahisi wewe tafuta mtu wa kumkodisha hilo shamba au lima mwenyewe
 
Last edited by a moderator:
Nimeshapata partner, nashukuru kwa michango yenu, ingawaje mingine ni ya kukatisha tamaa. Dunia imebadilika, sio mawazo yale yale kila siku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…