MKANDAHARI
JF-Expert Member
- Apr 7, 2011
- 5,727
- 6,615
Habarini ndugu zangu, kama kichwa kinavyoeleza hapo juu, natafuta mtu ambae yuko serious tuendeleze kilimo ambacho tayari nimeshakianza ila nguvu ya kukiendeleza imekosekana kwa vile hali yangu sio nzuri kwa sasa.
Ndugu zangu mwaka juzi na jana nimelima chekereni chini kidogo ya njia panda ya himo ukiwa unatokea moshi kwenda DSM. Hakikuniangusha maana kimenilipa vizuri tu.
Msimu huu nikajitosa tena kulima hoho na kitunguu, hoho sasa imeshaingia shambani ina kama mwezi hivi ila kitunguu ndio bado kipo kwenye kitalu ila wiki hii inayokuja ndio nilikuwa nimepanga kiingie shambani. Ila kuna matatizo flani hivi yalinikumba hapa katikati na kwa jinsi navyoona sitaweza kumudu gharama zake.
Kama yupo mtu ambae angependa kujumuika na mimi nipo tayari kuungana nae ili nisipate hasara maana nimeshaingia gharama sana kuanzia kwenye mbegu, kutunza mbegu na kuandaa shamba.
Naumia sana kuona kama nitashindwa maana yake nitakuwa nimepata hasara.
Kama yupo ambae yupo tayari njoo DM tuyajenge.
Natanguliza Shukran!