Natafuta Partner tulime naye Kitunguu

Natafuta Partner tulime naye Kitunguu

MKANDAHARI

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2011
Posts
5,727
Reaction score
6,615
Habarini ndugu zangu, kama kichwa kinavyoeleza hapo juu, natafuta mtu ambae yuko serious tuendeleze kilimo ambacho tayari nimeshakianza ila nguvu ya kukiendeleza imekosekana kwa vile hali yangu sio nzuri kwa sasa.

Ndugu zangu mwaka juzi na jana nimelima chekereni chini kidogo ya njia panda ya himo ukiwa unatokea moshi kwenda DSM. Hakikuniangusha maana kimenilipa vizuri tu.

Msimu huu nikajitosa tena kulima hoho na kitunguu, hoho sasa imeshaingia shambani ina kama mwezi hivi ila kitunguu ndio bado kipo kwenye kitalu ila wiki hii inayokuja ndio nilikuwa nimepanga kiingie shambani. Ila kuna matatizo flani hivi yalinikumba hapa katikati na kwa jinsi navyoona sitaweza kumudu gharama zake.

Kama yupo mtu ambae angependa kujumuika na mimi nipo tayari kuungana nae ili nisipate hasara maana nimeshaingia gharama sana kuanzia kwenye mbegu, kutunza mbegu na kuandaa shamba.

Naumia sana kuona kama nitashindwa maana yake nitakuwa nimepata hasara.

Kama yupo ambae yupo tayari njoo DM tuyajenge.

Natanguliza Shukran!
 
Miniko tayari kitakacholeta shida ni umbali kati yako na mimi. Nko mkoa wa mbali sana!!
Daaah, hii sasa shida! Trust ndio ngumu ila mimi sio tapeli maana naweza kuweka hata real identity kabisa
 
Mara nyingi ushirikiano ambao mmoja ameshaaanza tangia chini akakwamia njiani Humalizika kwa maugomvi na chuki kati ya hao washirika wa hilo jambo.

mara nyingi sana project hizi anapojitokeza mtu wa kuongeza nguvu mambo hutiki kwa asilimia zote,mziki wake huja kwenye kugawana faida.

Waanzilishi project hujionaga wao ndio kila kitu na bila wao wasingepata hiyo faida kwahyo huishia kuvutia kamba upande wake ili tu arudishe kwanza gharama zake kisha kale kaji faida kadogo kalichobaki ndio atataka mgawane wote tena.

ki ufupi Kuingia project ya namna hii yahitaji mtu ujitoe ufahamu,uwe na undugu wa damu damu na Yesu Kristo na bila kusahau usitoke mbali sana na ukoo wa Mtume Muhammad maana mwisho wa hili picha kama hutoki ktk ukoo wa hawa watu wawili.

unaweza ishia chinja mtu shingo au kumtenganisha miguu na kiwiliwili kwa hasira atazokupa,Wenye mioyo yenu Project hiyo hapo hii ni Betting tena BIKO.
 
Mara nyingi ushirikiano ambao mmoja ameshaaanza tangia chini akakwamia njiani Humalizika kwa maugomvi na chuki kati ya hao washirika wa hilo jambo...
Mimi siko hivyo bro, mimi nina roho yangu ya kipekee. Kuliko hii hela yote niliyowekeza hapa ipotee nipo tayari tugawane pasu kwa pasu kama atajitokeza. Afu kwenye project kama hii huwezi ingia bila maandishi. Au kama atajitokeza mtu ambae hataki ushirikiano nipo tayari kumuuzia anirudishie tu gharama nilizotumia tu basi!
 
Mara nyingi ushirikiano ambao mmoja ameshaaanza tangia chini akakwamia njiani Humalizika kwa maugomvi na chuki kati ya hao washirika wa hilo jambo...
Acha uchambuzi uchwara wa kutaka kukatisha tamaa wengine.
 
Habarini ndugu zangu, kama kichwa kinavyoeleza hapo juu, natafuta mtu ambae yuko serious tuendeleze kilimo ambacho tayari nimeshakianza ila nguvu ya kukiendeleza imekosekana kwa vile hali yangu sio nzuri kwa sasa.

Ndugu zangu mwaka juzi na jana nimelima chekereni chini kidogo ya njia panda ya himo ukiwa unatokea moshi kwenda DSM. Hakikuniangusha maana kimenilipa vizuri tu.

Msimu huu nikajitosa tena kulima hoho na kitunguu, hoho sasa imeshaingia shambani ina kama mwezi hivi ila kitunguu ndio bado kipo kwenye kitalu ila wiki hii inayokuja ndio nilikuwa nimepanga kiingie shambani. Ila kuna matatizo flani hivi yalinikumba hapa katikati na kwa jinsi navyoona sitaweza kumudu gharama zake.

Kama yupo mtu ambae angependa kujumuika na mimi nipo tayari kuungana nae ili nisipate hasara maana nimeshaingia gharama sana kuanzia kwenye mbegu, kutunza mbegu na kuandaa shamba.

Naumia sana kuona kama nitashindwa maana yake nitakuwa nimepata hasara.

Kama yupo ambae yupo tayari njoo DM tuyajenge.

Natanguliza Shukran!
Utalima njia panda Himo?
Nitumie mchanganuo wa gharama PM nichakate.
 
Duh..kilimo kinahitaji uvumilivu Tena Kama patina uwe karibu na Hilo shamba mkienda hatua kwa hatua ndio mtaona mafanikio.
 
Mara nyingi ushirikiano ambao mmoja ameshaaanza tangia chini akakwamia njiani Humalizika kwa maugomvi na chuki kati ya hao washirika wa hilo jambo.

mara nyingi sana project hizi anapojitokeza mtu wa kuongeza nguvu mambo hutiki kwa asilimia zote,mziki wake huja kwenye kugawana faida.

Waanzilishi project hujionaga wao ndio kila kitu na bila wao wasingepata hiyo faida kwahyo huishia kuvutia kamba upande wake ili tu arudishe kwanza gharama zake kisha kale kaji faida kadogo kalichobaki ndio atataka mgawane wote tena.

ki ufupi Kuingia project ya namna hii yahitaji mtu ujitoe ufahamu,uwe na undugu wa damu damu na Yesu Kristo na bila kusahau usitoke mbali sana na ukoo wa Mtume Muhammad maana mwisho wa hili picha kama hutoki ktk ukoo wa hawa watu wawili.

unaweza ishia chinja mtu shingo au kumtenganisha miguu na kiwiliwili kwa hasira atazokupa,Wenye mioyo yenu Project hiyo hapo hii ni Betting tena BIKO.
[emoji23][emoji23] nimependa ulivyoelrzea. nadhani Cha mhimu jamaa angeuza tu project. Shida nyingine mambo yasipo tik, alafu mtaji usirudi, ipatikane pesa kidogo, hapo ugomvi so mdogo.
 
Habarini ndugu zangu, kama kichwa kinavyoeleza hapo juu, natafuta mtu ambae yuko serious tuendeleze kilimo ambacho tayari nimeshakianza ila nguvu ya kukiendeleza imekosekana kwa vile hali yangu sio nzuri kwa sasa.

Ndugu zangu mwaka juzi na jana nimelima chekereni chini kidogo ya njia panda ya himo ukiwa unatokea moshi kwenda DSM. Hakikuniangusha maana kimenilipa vizuri tu.

Msimu huu nikajitosa tena kulima hoho na kitunguu, hoho sasa imeshaingia shambani ina kama mwezi hivi ila kitunguu ndio bado kipo kwenye kitalu ila wiki hii inayokuja ndio nilikuwa nimepanga kiingie shambani. Ila kuna matatizo flani hivi yalinikumba hapa katikati na kwa jinsi navyoona sitaweza kumudu gharama zake.

Kama yupo mtu ambae angependa kujumuika na mimi nipo tayari kuungana nae ili nisipate hasara maana nimeshaingia gharama sana kuanzia kwenye mbegu, kutunza mbegu na kuandaa shamba.

Naumia sana kuona kama nitashindwa maana yake nitakuwa nimepata hasara.

Kama yupo ambae yupo tayari njoo DM tuyajenge.

Natanguliza Shukran!
Naomba mchanganuo wa gharama PM kama bado haujapata serious patner.
 
Back
Top Bottom