Natafuta Partner wa Biashara ya Petro Station

Natafuta Partner wa Biashara ya Petro Station

HABARI, SAMAHANI MBONA PM YAKO INAGOMA? NAOMBA UNIPM TUZUNGUMZE ABOUT CERTIFICATES ZA LAZIMA KUWA NAZO ILI UPEWE LICENCE YA KUUZA MAFUTA
Mkuu kwa faida ya wengine ambao hapo baadae watahitaji kufanya hiyo biashara na kwa kuwa ni legal business ungetoa Elimu hapa jukwaani tuu...au wewe unaonaje vibali vinavyotakiwa ni hivi na vile na vinapatikana kwa kufuata utaratibu huu...
 
Mkuu naweza kukupa ushauri ukaifanya hiyo biashara mwenyewe bila kuungana na mtu, nimefanya hivyo na niko mbali sana kwa sasa. Kama utakua tayari ni PM.
Ushauri wangu utaulipia 1.5% of your workplan which is 3.75 millions.
Ntakupa ushauri na njia za kupita huku mipango yote nikiifanya mwenyewe hadi kazi yako inakamilika kwa 100%. Good luck
Aysee!
 
Akienda EWURA cha kwanza ataambiwa atafute certificate ya mazingira, eneo linatakiwa kufanyiwa Environmental Impact Assessment, na mchakato wa kufanyiwa EIA lazima awe na certificate kadhaa ili EIA ipite and then atapewa license, anyway nimeshamtafuta PM, kama nawewe mwekezaji karibu PM
Mkuu nikufuate PM kunielekeza jinsi ya kupata Certificate na license ? upo serious kweli ...
 
Mkuu huyu nilimfuata PM kwasababu post yake ilihitaji business partiner, mimi nikaona fursa kwangu kwa issue ya certificate, sasa ningeanza kumweleza humu nikaona sio busara maana tungetoka nje ya mada. Mimi nipo serious, angeuliza kuhusu process na certificates anazotakiwa kupata ningemwelekeza humuhumu kwa faida ya wote
Mkuu nilikuja kukuelewa baadae sana upo sawa kabisa, poa.
 
Natafuta serious Partiner wa kufanya nae biashara ya Petrol Station. Nina kiwanja tayari chenye ukubwa wa sqm zaidi ya 3000,eneo lina future ya biashara kwa kuwa hakuna kituo cha mafuta maeneo jirani,Kiwanja kimeshaingizwa ktk ramani za mipango miji imebaki kufainalize some process and payments, mashine ninazo jumla zipo tano 5 za petrol,diesel na mafuta ya taa..Budget yote ya makadirio ilikuwa kama 250 milioni,niliandaa workplan and budget mwenyewe,tunaweza kuziboresha na kuandaa business plan..
Any serious person namkaribisha PM tuzungumze.Awe na capital ya kutosha,mipango mizuri yabiashara na awe business oriented person.Its a serious deal!
Npgie tuongee 0784616544
 
Back
Top Bottom