Natafuta partnership kwenye biashara ya Clearing and Fowarding

Natafuta partnership kwenye biashara ya Clearing and Fowarding

Naomba kufahamu vitu vifuatavyo:-

1. Una bond ya kiasi kwa ajili ya transit goods.
2. Una container deposit waiver kwenye shipping line ngapi?

Naweza kufanya kazi na wewe kama nitaridhika na hayo majibu.

NB: nitakulipa agency fee tu iwapo tutakubaliana .

Nina wateja wa
LUSAKA
MAZABUKA
NDOLA
CYANGUGU/KAMEMBE

Thanks
 
Naomba kufahamu vitu vifuatavyo:-

1. Una bond ya kiasi kwa ajili ya transit goods.
2. Una container deposit waiver kwenye shipping line ngapi?

Naweza kufanya kazi na wewe kama nitaridhika na hayo majibu.

NB: nitakulipa agency fee tu iwapo tutakubaliana .

Nina wateja wa
LUSAKA
MAZABUKA
NDOLA
CYANGUGU/KAMEMBE

Thanks
Mkuu nimekujibu kwenye meseji
 
Asante sana mkuu kwa ushauri wako
Wewe cheza na madalali wao wana wateja na wajanjawajanja sana. Utakuwa unauziwa kazi, sharti moja usiwe na tamaa kabisa unaweza kuta unapata 20% ya hela anayopata kwa kumsumbua mteja wake. Wewe jua market inawapa kiasi gani na uwe faster kutimiza kazi zao na uwajue wanalialia sana kutaka kupunguziwa.

Wao wana uwezo mkubwa wa kutafuta wateja ila hawana vigezo vya kufungua kampuni na hata wakiwa navyo kampuni zitakufa kirahisi. Mpaka unakuja kuzoea na kupata wateja wako mwenyewe watakufikisha hatua fulani ila huwezi wakimbia kwenye kazi hiyo.
 
Nenda pale Posta lile jengo lao kuukuu ukutane na vishoka wasumbufu, matapeli, wahuni na wababaishaji. Fanya nao kazi kwa muda uwe unawapa commission nzuri, muda ukienda utawachuja nani anafaa.

Unaweza tumia madalali ambao wakizingua unawatema ila sio partnership. Umekosea kuanzisha kampuni bila wateja, ilibidi uwe kishoka/dalali kwanza.
Addition
Kama wateja wake ni wazambia au wamalawi tafuta connectuon ya wale ma agent wao wale ambao wanawaagizia magari kuwa nao na urafiki wale kazi zitakuja naonaga wanaofisi nyingi sana kasumulo/tunduma

NB: tumia pisi kali hapa kuwapata hawa ma agent

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Naomba kufahamu vitu vifuatavyo:-

1. Una bond ya kiasi kwa ajili ya transit goods.
2. Una container deposit waiver kwenye shipping line ngapi?

Naweza kufanya kazi na wewe kama nitaridhika na hayo majibu.

NB: nitakulipa agency fee tu iwapo tutakubaliana .

Nina wateja wa
LUSAKA
MAZABUKA
NDOLA
CYANGUGU/KAMEMBE

Thanks
Ukishampata mbia usisite kunitafuta mzee wa DP world nikusaidie kuwahisha kuchomoa mizigo dox...
 
Wakuu bado sijapata mtu wa kupatner mwenye wateja
Kama walivyoeleza wadau hapo juu, cheza na madalali.

Kutafuta partner tena mwenye wateja sidhani kama ni rahisi.

Partnership utafanya endapo unataka kukuza mtaji wa kampuni kwa kuongeza nguvu kwenye uwekezaji na usimamizi

Ukishakuwa na wateja kipaumbele kinabadilika, kama ni mtaji ungejikuta unaanza kufikiria kukopa bank, na kuongeza wafanyakazi labda.
 
Wakuu bado sijapata mtu wa kupatner mwenye wateja
Vigumu sana kupata.
Kampuni ya clearing hata milioni 7 unafungua, wangapi wanayo hiyo hela na awafungui kampuni. Kitu cha muhimu ni wateja, ukiwa na wateja unaweza pata hela kuliko mwenye kampuni.
Hapo ukikaa mwaka ukalipa tax, rent na vitu vingine utajikuta unaoperate kwa faida kidogo. Dalali mwenye wateja atakuzidi ndio maana madalali wengi hawawazi kuanzisha kampuni. Dalali akipata commission yake halipii kodi sijui leseni wala ushuru. Na dalali ana mwanya wa kumsumbua mteja na kumlipisha gharama ya juu zaidi.

Mwenye wateja akija kwako anajifunga, ukitoa makato na malipo mengine atapata hela ndogo kuliko anayopata sasa, na hiyo hela mtagawana. Hakuna partner wa kuja kupata hela pungufu ya anayopata. Ukitumia madalali unaweza usipate wateja wako na kazi ukafanya kwa faida pungufu zaidi.
 
Back
Top Bottom