Dah! nafiliri mtoa post anahitaji msaada zaodi ya kujifunza ujasiriamali.
Kwa uzoefu nilionao na nikikumbuka maneno wa msanii maarufu 'Mjomba kuwa asiyejua aendako hawezi kupotea' Mtoa post unapaswa kutambua yafuatayo.
1:Ujasiriamali unaoutaka una nyanja nyingi sana,nyingine unazozipenda na nyingine usizozipenda.
2:Unapaswa kuchagua nyanja zile tu unazozipenda.Hii itakusaidia kufanya vizuri na kutopoteza muda kwa mambo ambayo huna 'interest' na pengine hutokuja kuyatumia maishani.
3:Fuata ushauri wa wadau waliokupatia ukijua unataka aina gani ya ujasiriamali na mahali bapo unaweza kupata mafunzo ya ujasiriamali unaoutaka.
Kila la kheri.
Nikweli mkuu wewe umeweka wazi,maana siku hizi kumeakuwa na vituo kibaoo vya mafunzo haya ila baadhi yao vinaharibia wenzao majina,maana wao wanafanyakila kitu lakini juu juu saana mtu anatoka hana hata moja,wakiishapiga hela yao moto.
Hembu wenye kujua mnijuze yafuatayo,maana najipanga mwakani ku attend mafunzo binafsi na mie katika Theory na Pratical.
Wapi ni best kwa Mafunzo ya Ujasiriamali katika:-
-Ufugaji wa Samaki (Sato)
-Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji
-Kilimo cha Matunda(Embe,Mapapai,Passion,Machungwa nk)
-Kilimo cha mbogamboga
-Usindikaji wa Asali na uhifadhi wake
-Biashara ya kutengeneza Mikate,Bakery kwa ujumla
-Ufugaji wa Ng`ombe wa Maziwa