kwa makadirio tu itahitajika 100,000,000+ kwa, hali ya mifuko ya wengi + uaminifu na watanzania tulivyo wataalam kwenye risk cakculation utaambulia kuungwa mkono kwa kauli tu badala ya vitendo.
nashauri upange mradi wako ktk hatua/phases hata 4. kama unaanza na banda la banzi+nguruwe 10 utakaowauza hai itapendeza.
baada ya kuona faida panua banda, ongeza mbegu mara mbili au tatu
hatua ya 3 jenga miundombinu kwa kutumia faida na kuanza kusaka wadhamini+wadau wa kuunga juhudi tyr ukiwa na kianzio.
mwisho panua soko lako ulilolenga (hotels), vyombo na mabanda ya kisasa sanjari na usajili ktk mamlaka husika ukiwa umeshaonja matunda.
nchi yangu ya Tanzania imejaaliwa watu wenye vipawa vyote, wajuaji, wakatisha tamaa, werevu wa kusigana, matapeli wa kila hali, washirikina na non risk takers (sijui niisemeje kwa kiswahili) . usitegemee atokee mtanzania akuamini kwa maneno matupu tu hayo na hesabu zako za kisomi (iweke sawa hesabu za makaratasi) badala yako watakuwela kundi moja na wale inspiration speakers; wanahamasisha kilimo cha biashara mf. bustani kuwa unatumua milioni 1 ulivuna unapiga milioni 10. amini bure ekari 3 bila hatua uliyokwishapiga kuelekea wazo lako, hazitoshi kumshawishi mtu amwage pesa.
mimi ni miongoni mwa watanzania wagumu kumuamini msomi wa nchi hii kwa taaluma ya uchumi. maramia nimwamini mwanasiasa na ahadi zake maana huwa nimejindaa kisaikolojia kwa kitakachofuata, huwa wanaanguka lakini baada ya kujaribu na hakika hututia matumaini kuwa awamu ijayo watafanikisha. laiti maafisa ugani na bw/bi. kilimo wangekuwa lau na mashamba darasa ya lau rbo heka kutuwekea elimu zao kutoka makaratasi kuwa vitendo ingefaa kunibadili.
naungana na mchangiaji hapo juu.
sisi ambao hatukusoma/hatukubahatika kuajiriwa hakuna fursa ambazo hatujajaribu. kilimi, ufugaji, biashara, viwanda vidogo (vyerehani, mashine za, mbao na nafaka) we speak frankly from experience. ni msomi tu anatuchukulia poa kwa vile anatuzidi hesabu
hitimisho :
unda kundi la jamaa zako pengine school mates,members wa grp za whatsap, work mates mchangishane hata 500,000 au m1 kwa watu kama 10/20 mjenge credibility, hapo tutawapokea kirahisi hata kwa kutuuzia hisa (chonde tu zisije kuwa km za voda).
KILA LA KHERI!