Natafuta Serious Partner wa Kuanzisha Mradi Mkubwa Wa Nguruwe Tanzania

Daaah...! Nina wazo hilo muda mrefu mkuu,na ardhi nilishanunua. Lakini ardhi yako iko mahala pazuri kuliko mimi,nafikiri tukikubariana. Ni wazo zuri,halina mjadala linavusha
 
Haa haa haa karibu Sana Kiongozi. Hakuna linaloshindikana. Nimefurahi kusikia Una wazo kama hili. Ni-PM Kwa majadiliano zaidi.
Daaah...! Nina wazo hilo muda mrefu mkuu,na ardhi nilishanunua. Lakini ardhi yako iko mahala pazuri kuliko mimi,nafikiri tukikubariana. Ni wazo zuri,halina mjadala linavusha
 

Nimekupenda bure
 

Watu mna madini Kama yote.

Nimependa maoni yako.
 
Watu mna madini Kama yote.

Nimependa maoni yako.
Nyongeza kidogo.

Mimi nipo mkoani ifakara, Morogoro. Ufugaji wa nguruwe kwa hapa ni rahisi kuliko sehemu yoyote nchini. Unapata pumba za Mpunga kwa bei ya kutupa. Maana hapa ndio wazalishaji wakubwa wa mpunga. Kg 70 ya pumba napata kwa shs 2500 hapo nishamlipa na mjazaji. Kwa nilivyo alwatan naweza kupata bure.

Mashudu ya alizeti yapo kwa wingi, Pumba za mahindi zipo kibao kwa kifupi ufugaji wa hapa ni rahisi. Ila changamoto zipo. Mimi sifanyi ufugaji wa kuzalisha, nafuga kuendeleza. Nanunua kwa kuchagua nguruwe wazuri ambao hawajadumaa.

Natengeneza chakula cha mwezi mzima kinanigharimu kama tsh 200k na kinatosha kulisha nguruwe 80-100 kwa mwezi. Ila pumba za mpunga zinazidi kwenye huo mchanganyiko.

Nachanganya pumba za mahindi, Mashudu ya alizeti, pumba za mpunga, chumvi, pig mix wakati mwingine na dagaa. Matengeneza gunia 30 zinatosha kulisha mwezi mzima. Nawalisha Ahsubuhi na jioni. Wanapewa majani kila baada ya siku tatu.

Ufugaji wangu ni kama kibubu. Nikiuza ndio nimevunja.
 
Ahsante 072, nashkuru Kwa kunipa taarifa na uzoefu wako. Utakuwa wa msaada katika kupata vyakula toka huko kwenu.
 
100 Millions ukafungue mradi wa ufugaji wa nguruwe! This is a joke. Mkuu nguruwe wala hawaitaji nguvu kubwa kiasi hicho. Mbona ni rahisi sana, labda kwa sababu huko jamaa alipo ni mbali.

Pili mradi kama huo hauitaji kuwa na partners, unauendesha mwenyewe tu. Ngoja nikupe mfano mzuri kabisa.

1. Kwa kuanza kwa kuwa tayari ana utayari, anajenga banda la mbao/banzi. Liwe na urefu wa futi 10-12 kwenda juu. Akate vyumba vya kutosha kukaa nguruwe wa5 kila chumba. Hii maanake atajenga banda la bati 40. Unapauwa kwa upande mmoja. Yaani linamwaga maji upande m1.
Wastani hili lita gharimu kama 3 millions. Hapa utatumia nguzo na mbao au banzi.

Nguruwe ananunua 50 kwa wastani wa tshs 70-80k. Kazi imeisha. Anaanza kulisha anasubiri soko. Sasa ukiangalia hapo harama haiwezi kuzidi 15ml.
 
70kg kwa 2500/=???
Vp mashamba yakununua wanauzaje huko kwa ekari?
Upatikanaji wa maji ya ardhini ukoje?
 
70kg kwa 2500/=???
Vp mashamba yakununua wanauzaje huko kwa ekari?
Upatikanaji wa maji ya ardhini ukoje?
Mashamba kama ni nje kabisa ya mji ni 800000-100000 kwa heka. Mashambani kabisa unaweza kupata mashamba heka 10 kwa mpaka 3000000.

Maji ya ardhini yapo mengi. Kila nyumba hapa ina kisima cha kupampu. Wanyeji wanaita mdundiko. Kila mtu anajichimbia tu. Tena kwa gharama nafuu. 350000 unapata kisima chako.
 
Mkuu nakupa tahadhari, RUDIA RESEARCH YAKO MKUU. Alafu Nguruwe hawafugwi kando ya vyanzo vya maji hasa hawa wa large scale farms sasa hapo umejipanga vipi?

Anyway all the best
 
Nimefurahi sana kukutana na uzi huu na nina siku nyingi sijaingia JF.
Kwa upande wangu naweza kukujoin kwa kuwekeza kwenye teknolojia ya kuzalisha chakula cha mifugo hao kwa kupunguza gharama ya malisho zaidi ya 50%
Niwe wazi ni kwamba kwa sasa najishughulisha zaidi na ufundishaji wa teknolojia ya Hydroponics Fodder pamoja na kilimo cha Azolla. Kwa pamoja yote hayo ni kwa ajili ya kupunguza gharama za malisho ili kuongeza faida kwa mfugaji.
Kama utakuwa umenielewa (wewe mtoa mada) tunaweza kuwasiliana zaidi.
 
Kama sijakupata hivi au ni typing error.umeandika laki8 mpaka laki 1.huku kwa ekari 10 kwa m3 ambayo ni sawa laki3 kwa kila ekari.
 

Hivi Ifakara ishakuwa Mkoa...??

Ila hongera kwa ufugaji usio na gharama Kama wa mijini hasa dar...kuku tu wanakutoa hela Hadi unaomba pooo..

By ze way vipi mafuriko huko??
 
Hivi Ifakara ishakuwa Mkoa...??

Ila hongera kwa ufugaji usio na gharama Kama wa mijini hasa dar...kuku tu wanakutoa hela Hadi unaomba pooo..

By ze way vipi mafuriko huko??
bado haijawa mkoa. Soma post yangu vizuri. Nimesema nipo ifakara morogoro. Kuhusu mafuriko Juzi kati ilikuwa balaaa.
 

Bei za wapi hizo mlongo namimi nikanunue aisee.
 

🤔😀.Hao nguruwe unawapeleka sokoni wakiwa na umri gani?!
Wanakuwa na uzito gani wanapoenda sokoni!!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…