Natafuta Serious Partner wa Kuanzisha Mradi Mkubwa Wa Nguruwe Tanzania

[emoji848][emoji3].Hao nguruwe unawapeleka sokoni wakiwa na umri gani?!
Wanakuwa na uzito gani wanapoenda sokoni!!?
Sisi hatupeleki sokoni. Kuna wateja wanakuja toka Dsm, unampeleka bandani anachugua anaona wanamfaa. Tukiafikiana bei analipa anachukua mzigo wake.
Soko kubwa ni Dsm.
 
Ni sawa.Nilikuwa nna maanisha unawauza wakiwa na umri gani na uzito gani!!
Ila nimekuelewa;kwenu haijalishi umri wala uzito wa mnyama;yawezekana pia haijarishi ni gharama kiasi gani umetumia kuwalea hao nguruwe🀭.Hao jamaa wakija bandani wakachagua na mkaelewana basi wanachukuaπŸ˜ŠπŸ€”!Nadhani namna hiyo ni kawaida katika ufugaji vijijini;ufugaji wa kujikimu. Kawaida huko vijijini mtu kuuza nguruwe wakiwa na umri wa mwaka mmoja au zaidi bali wakiwa bado wana uzito mdogo.Kwa mtu anaetaka kufuga nguruwe kibiashara labda anahitaji kufanya zaidi ya hivyo🀝🀝🀝
 
Hapana. Tunachofanya, ni kuwa nguruwe wanakuwa na wastani wa kg 80-100. Namoa pei nayotaka, mara nyingi ni 300k mpaka 350k. Akiingia bandani anachagua wanaomridhisha. Kwa kuwa wale nguruwe walinunuliwa wakiwa wanalingana basi lazima apate wengi. Akichukua 30 tu sikosi 10m.
 
Hongera sana kijana kwa maono yako[emoji122][emoji122]
 
Ahsante Tutor B. Ntawasiliana nawe. Nimeona namba yako.
 
Umeelezea vizuri..!

Mimi nimfugaji , na tuna chama cha wafugaji wa nguruwe wa kisasa kinaitwa TAPIFA, HQ ni morogoro. Ukiweza fika hapo, unaweza tafuta watu mkainvest now. But kutoa ardhi bila kuwa na fedha ni kazi bure. Nguruwe 50 sio msikhara. Inabidi uwe na sio chini ya 10M. Na unaanza kuona matunda yake baada ya miaka 2-3 kama ukifuga vizuri,
 
🀣🀣🀣
Words are opinions;action is the only truth🀣🀣

🀣🀣
 
Mkuu uko mkoa gani?Ngurue wanatafutwa sana maana nakumbuka kipindi niko moshi,kulikua kuna wadau wanatoka Dar kutafuta ngurue,na walituambia kuna kipindi wanaenda mpaka mbulu kutafuta ngurue,mama yangu alikua mfugaji mzuri sana,na Ngurue wa 70kg alikua anamuuza 350k,hii ni kwa wastani wa 5000kwa kg.
Na pia alikua anasuply kiwanda cha soseji Arusha,na hawa wa soseji arusha walikua hawana longolongo,ukiwa na breed nzuri,na ngurue wa kiume uwe umemuasi toka akiwa na miezi mitatu,amasivyo nyama inakua na harufu ambayo madume wanakua nayo,na kwenye soseji hawataki iyo harufu.Ngurue wakifika kiwandani tuu,hela mama anawekewa CRDB Chap!
So demand ya Ngurue in kubwa sana has a Arusha,Moshi,Dar na Mwanza
 
 
Nguruwe ni nyama tamu sana kwa kweli, kuhsu madhara, kitu chochote ukikitumia kupita kiasi kina madhara, hata nyama ya ng'ombe ina madhara... tusivuke mipaka, inapoishia haki yako, ni mwanzo wa haki ya mtu mwingine
 
Ngurue mzuri ni wa miezi tisa toka wamezaliwa ukimtunza vizuri anakua na kilo kati ya 65-75,na nivizuri ukawaasi wakiwa na miezi mitatu
Na wanahitaji maji asikudanganye mtu hasa kipindi cha joto ile mida ya mchana unawamwagia maji
Kijijini kwetu tuko karibu na mto na mzee kamfungia pump mama kwa ajili ya kuvuta maji kwa ajiili ya ngurue na maboga,maana mama hua anapanda maboga kwa ajili ya ngurue, maboga na migomba na majani shambani,vinampunguzia sana gharama ya chakula
[emoji848][emoji3].Hao nguruwe unawapeleka sokoni wakiwa na umri gani?!
Wanakuwa na uzito gani wanapoenda sokoni!!?
 
Hao wa kushirikiana nao unahitaji mtu mmoja ama ata kama ni 20. Namaanisha huyu katoa kiasi hichi yule kile mpaka kupata kiasi kinacho itajika.
 
Wanaweza wakawa zaidi ya mmoja. So far kuna watu tayari wameshaonesha interest ya kufanya kazi zaidi ya watu wawili. So tunakaribisha wadau wengine.
Hao wa kushirikiana nao unahitaji mtu mmoja ama ata kama ni 20. Namaanisha huyu katoa kiasi hichi yule kile mpaka kupata kiasi kinacho itajika.
 
Nipo morogoro. Wilaya ya kilombero mjini ifakara.
 


Mkuu,hongera sana kwa kuwa na mawazo mazuri sana ya ubunifu wa mradi unaoweza kutoa ajira si kwako pekee bali kwa ushirika.

Kwa fikra yangu; ni kwamba mradi huo siyo mzuri kwa jamii kwani nguruwe hutumiwa zaidi kwa ajili ya kitoweo, watu wengi hawajui kwamba pamoja na madhara mengine yanayosabishwa na nyama ya nguruwe kama cancer pia ulaji wake huambukiza "USHOGA", angalia Mashoga wengi historia yao utakuta walianza kula nyama ya nguruwe kwa wingi toka wakiwa wadogo/watoto kama (staple food).

Kifupi ulaji "sana" wa nyama ya nguruwe inachangia "sana"watu kuwa mashoga.

Ushauri wangu (with due respect), Tafuta mradi mwingine.

πŸ™πŸ»πŸ™πŸ»
 
Pork meat is one of the best meat ever!!
Usidanganye watu.
Kuna joint moja iko nyamanoro,kabla hujafika njia ya kupandisha kawekamo kuna kiti moto moja matata Sana'a!This wkend lazima nimshtue boss tukatandike kilo na ndizi nne.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…