natafuta shule ya 0 level

mshewa2

Member
Joined
Oct 30, 2012
Posts
77
Reaction score
12
natafuta shule ya private ya o level kwa ajili ya my niece nataka. shule ya bei rahisi as sina kipato kikubwa,iwe laki 6-8 kwa mwaka,kila shule ninayoulizia ni kuanzia milion na zaidi,shule za boarding.
 
natafuta shule ya private ya o level kwa ajili ya my niece nataka. shule ya bei rahisi as sina kipato kikubwa,iwe laki 6-8 kwa mwaka,kila shule ninayoulizia ni kuanzia milion na zaidi,shule za boarding.

Pole sana Mshewe2. Najaribu kujiweka katika viatu vya miguu yako. Shule nzuri za Boarding ni ghali sana zile ambazo kidogo ni reliable kiufundishaji na maadili. Za bei yako hiyo zinaweza kuwepo ila ubora wake ni lazima uuangalie sana. Again pole sana, haya ndiyo madhara ya kubinafshisha kitu muhimu kama elimu na hakuna any control mechanism ya ada na ubora kwa kuwa wenye hizo shule ndiyo wahusika wa kuweka hizo sheria!! Wote wana conflict of interest!! Sasa mtu yuko Wizara ya elimu halafu ana shule au ana share katiks shule, ni tabu sana!! Tutakukumbuka sasa baba wa Taifa hili hayati Mwalimu J. K Nyerere. Tulikuwa hatuna ubaguzi wa elimu na wote tulikuw ana akili sana!! Siku hizi tunatengwa!!
 
Kuna shule moja ipo Iringa inaitwa St. Thomas Nyabula secondry ipo wa 9km kutoka ipogolo na inafikika kwa daladala, inamaadili ya katoliki. Wastan wa kuhama darasa ni 50% chini ya hapa anarudia au ahame shule. Ni ya boarding na ada ni laki 8.5 ndo imetoa form 4 kwa mara ya kwanza. Mitihani yote ya kimkoa ipo kwenye kumi bora. Jaribu hii mkuu, ipo nyingine inaitwa consolata secondary inasifa sawa na hii ila wastan wao ni 45% na ada laki 9.5, ipo baada ya kumaliza kona za mwangata unapoelekea Ruaha National park. Ni ya boarding
 

thanks a lot ,let me check me them kuna jamaa yangu yuko iringa,hili swala la shule gumu wa Sie,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…