Natafuta sinema za Kuhuzunisha


Hilo sinema nitalipata wapi mkuu? Manake hilo movie lilileta sekeseke kubwa na limesababisha Ulimboka ajifiche/afichwe mpaka sasa sijui yuko wapi?
 
Jaribu kuitafuta Border Town ya Jeniffer Lopez na Tears of the Sun yake Bluce Wills na Monica Belluci.
 
Wadau, kama kichwa cha habari kinavyojieleza, ni kwamba natafuta sinema ambazo zinahuzunisha kiasi cha kumtoa mtu machozi.

Nawasilisha.

Angalia hii inaitwa Bangkok Hilton,kama hukuhunika na kutoa machozi,basi jua hata ukipata msiba wa mzee wako hutolia.
 
Hekima, nguvu ya imani, njia panda,nzowa, kichupa, Anne Marie na majuto, zote hizo toka bongo movie, hautojutia mkuu ni noumaaa
 
Hilo sinema nitalipata wapi mkuu? Manake hilo movie lilileta sekeseke kubwa na limesababisha Ulimboka ajifiche/afichwe mpaka sasa sijui yuko wapi?

Utalipata Makao Makuu Ya Jeshi La Polisi na Ukienda Tu Pale Muulize IGP Mpya EM Atakupa tu na Hata Zingine Pia Utazipata Kwa Kamanda Kova Na Kama Kote Huko Utaikosa basi Nenda Makao Makuu Wizara Ya Mambo Ya Inside Kitengo Cha Intelijensia Na Watakupa tu Tena Bila Matatizo na Huku Wakikuchekea na Kukufurahia Sana..............!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
The Confession of a marriage counselor
 
Wadau, kama kichwa cha habari kinavyojieleza, ni kwamba natafuta sinema ambazo zinahuzunisha kiasi cha kumtoa mtu machozi.

Nawasilisha.
Kuna movie niliangalia miaka mingi kidogo kama 25 iliyopita kuna kijana alimchumbia mwanamke aliyekuwa na uhusiano na baba yake nafikiri yule mchumba wake alikuwa anafanya kazi ofisi ambayo baba yake huyo kijana alikuwa akifanya.

Sasa mwisho wa siku kuna watu walimlengesha yule kijana bila kujua alienda kufumania lodge ghorofani kwa taharuki Yule kijana alianguka toka juu ya ngazi za ghorofa mpaka ground floor akafa, yule mzee alishuka chini akiwa uchi kwa kuchanganyikiwa na kulia sana yule dada akapita katikati yao na kusepa lile sakata likafika kazini kwa yule mzee akafukuzwa kazini tafadhali naomba mwenye kujua title ya hii movie, nawasilisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…