Kama upo serious nenda Dar kariakoo ukaulizie hasa kwa waarabu ambao wanauza dawa za asili. Pia waarabu ni wanunuzi wazuri sana wa asali kwa maana ni dawa na wanaisafirisha kwenda nchi za kiarabu kwa kua kule hakuna hiyo kitu na nchi zao ni jangwa tu. Sina uhakika na bei ya asali wa nyuki wa kawaida ila kuna wakati mie nilifuatilia bei ya asali ya nyuki wadogo ambayo ilikuwa ikinunuliwa kwa 15000 kwa lita. Kwa hiyo hiyo inaweza ikawa sio zaidi ya 8000 kwa lita coz wauzaji wengi huuza kwa 10000 kwa lita. Nenda Dar mkuu ukafanye research na upate mteja wa uhakika kwani hata wao hupenda mtu ambae ana supply kwa uhakika.