Natafuta soko la mayai ya kisasa

chaArusha

Member
Joined
Mar 24, 2011
Posts
88
Reaction score
31
Habari wakuu.

Mimi ni mtu ninayevutiwa na ujasiriamali, sasa niliwahi kusikia kuhusu biashara ya ufugaji wa kuku wa mayai. Nilianza kwa majaribio kuku 300 tokea April mwaka huu, hivi sasa wameanza kutaga kidogo kidogo.

Hadi ninapoandika uzi huu, ninaokota trey 3 kwa siku lakini wana dalili za kuongeza kiwango. Sasa naombeni mnisaidie jinsi ya kupata soko. Mimi ninaishi Madale na kituo changu cha kupandia gari ni Tegeta Nyuki.

Ninauza trey kwa 6500, kama kuna mwenye chochote cha kunisaidia naombeni.
Nawakilisha
 
Hongera anzia kwa watu wanaokuzunguka wenye chipsi, vimgahawa. Pia ulizia tegeta kama kuna wakala wa jumla. Unavyopata bill jirani inakupunguzia gharama kusafirisha.

Ukishindwa kuna wakala ilala sokoni na bagamoyo sokoni ukipeleka kila wiki mbili au moja itakuwa poa
 
6500 kwasasa ni bei kubwa sana. Wenzako wanauza 5500 mpaka 5000
 
Kiongozi jambo la kwanza la kufanya kabla ya kuanzisha mradi wowote ni kutafuta walaji (soko). ninachokushauri jaribu kuzungukia kwenye maduka wanayouza vyakula, kwenye vibanda vya chips na pia kama ni mfanyakazi pia ulizia kwa wafanyakazi wenzako...taratibu utapata soko.

But angalizo ni kuwa ulizia kwanza bei ya soko kwa sasa ikoje...kwa ujumla bei sasa ya mayai imeshuka sanaa tu, kuna wadau walisema kwa dar sasa ni 4500 mpaka 6000. na kwa sababu wewe ndo wanaanza kutaga kwa kawaida mayai huwa madogo....baada ya mwezi mmoja mpaka miwili mayai ndo huwa saizi ya kawaidas.

ANAGLIZO. kama umeanza kufuga mwezi wa nne na kama sasa ndo wanataga trey 3 kwa siku ie 90 out of 300 kuna kosa la kiufundi kubwa tu limefanyika kwa hao kuku...ilibidi wawe wanataga more than 85% sasa wewe ni kama 30% wakati hiyo percent ni katika wiki ya 21 au 22 ya umri wao.

USHAURI WANGU; jaribu kuwasiliana na wataalam wa mifugo au wafugaji wenzako kwa ushauri zaidi
 
[Kiongozi jambo la kwanza la kufanya kabla ya kuanzisha mradi wowote ni kutafuta walaji (soko). ninachokushauri jaribu kuzungukia kwenye maduka wanayouza vyakula, kwenye vibanda vya chips na pia kama ni mfanyakazi pia ulizia kwa wafanyakazi wenzako...taratibu utapata soko.

But angalizo ni kuwa ulizia kwanza bei ya soko kwa sasa ikoje...kwa ujumla bei sasa ya mayai imeshuka sanaa tu, kuna wadau walisema kwa dar sasa ni 4500 mpaka 6000. na kwa sababu wewe ndo wanaanza kutaga kwa kawaida mayai huwa madogo....baada ya mwezi mmoja mpaka miwili mayai ndo huwa saizi ya kawaidas.

ANAGLIZO. kama umeanza kufuga mwezi wa nne na kama sasa ndo wanataga trey 3 kwa siku ie 90 out of 300 kuna kosa la kiufundi kubwa tu limefanyika kwa hao kuku...ilibidi wawe wanataga more than 85% sasa wewe ni kama 30% wakati hiyo percent ni katika wiki ya 21 au 22 ya umri wao.

USHAURI WANGU; jaribu kuwasiliana na wataalam wa mifugo au wafugaji wenzako kwa ushauri zaidi ]

Asante kwa ushauri, lakini si kwamba wako wote 300, wengine walikufa na waliopo bandani ni kati ya 240 hadi 250, ile idadi ya 300 nilichukulia tu kama ndo niliowachukua na kuanza kuwafuga
 
Nipo tayari lakini nimfanyie 6000 tufanye biashara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…