Asante kwa mchango wako wa mawazo mkuu, gharama ya wastani kulima ekari moja kwa tractor ni 40,000/= . Shamba jipya ni ngumu kutumia tractor, option kusafisha kwanza kwa mikono ambapo bei ndo hiyo inakuwa 60,000/= kwa ekari moja. Pengine kwako hiyo ni pesa ndogo sana ila ni muhimu kutambua kuwa unapofanya biashara faida inategemea sana gharama za uzalishaji, na hiyo 60,000/= nayo imepatikana kwa kazi ngumu na kujibana vilevile. Mimi nilidhani ni vizuri kugawana hiki kidogo na watanzania wenzetu kwa kupeana ajira hizi katika kilimo, kuna taarifa kuwa katika baadhi ya sehemu wakenya wanakuja wanafanya hizi kazi mashambani. Samahani kama umekwazika mkuu!!