John Kachembeho
JF-Expert Member
- Dec 29, 2013
- 560
- 388
Watafute wagogo huwa wanachapa kazi sana, kuna mmoja alinifyekea shamba langu la heka 10 kwa week 2 na nusu tena peke yake. Ila tatizo sio wakaaji akimaliza anasepa zake
hekari 30 ujue ni sawa na eka 75!. unafikiri wwwatu wanne wataziweza?
Trekta ni mkombozi kwa sehemu yenye matatizo ya nguvu kazi.
hekari 30 ujue ni sawa na eka 75!. unafikiri wwwatu wanne wataziweza?
Asante kwa mchango wako wa mawazo mkuu, gharama ya wastani kulima ekari moja kwa tractor ni 40,000/= . Shamba jipya ni ngumu kutumia tractor, option kusafisha kwanza kwa mikono ambapo bei ndo hiyo inakuwa 60,000/= kwa ekari moja. Pengine kwako hiyo ni pesa ndogo sana ila ni muhimu kutambua kuwa unapofanya biashara faida inategemea sana gharama za uzalishaji, na hiyo 60,000/= nayo imepatikana kwa kazi ngumu na kujibana vilevile. Mimi nilidhani ni vizuri kugawana hiki kidogo na watanzania wenzetu kwa kupeana ajira hizi katika kilimo, kuna taarifa kuwa katika baadhi ya sehemu wakenya wanakuja wanafanya hizi kazi mashambani. Samahani kama umekwazika mkuu!!
nafikiri hector waswahili tunaita heka!?.mkuu mahesabu ya wapi hayo?? Hector ndo hekari kwani?
Tunaomba utusaidie contact za wagogo Mama yake P
nafikiri hector waswahili tunaita heka!?.
Sorry sijaingia humu siku nyingi, ntawawekea contact ya huyo mmoja mnaweza kumuomba awatafutie wenzake mana kwa sasa yeye yuko kwenye shamba la rafiki yangu huko tanga
Asante sana Mama yake P, nilibahatika kupata wagogo kadhaa wako wanapiga kazi!
Nahitaji namba yako mkuutpmazembe, namimi nalima huko handeni Komkonga. Nakabiliwa na tatizo la nguvukazi pia, kama unavyojua ilivyo vigumu kuwapata wenyeji na ukizingatia na hali ya mvua inavyonyesha sasa inakuwa ngumu kuwashawishi wakubali kuingia shambani. Labda tushirikiane tu kutafuta watu wa mikoani kama ulivyoamua tayari, ila nadhani namna nzuri ya kuwalipa ni kwa kipimo cha kazi. Mfano mimi pale nimekuwa nalipa 60,000/= kwa kila ekari moja inayofyekwa na kulimwa (Bado ni pori sehemu kubwa). Cha kufanya ni kuwatengenezea kambi hukohuko shambani, gharama za chakula ni sehemu ya malipo ya kazi yao. Kilimo kikiisha wanarudi kwao kupumzika hadi utakapowahitaji tena. Challenge kubwa ni namna ya kuwapata, tuwasiliane kwa pm tushirikiane kuwapata kwa wingi!