Natafuta vijana wa kuniuzia juice

Ongeza24

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2023
Posts
396
Reaction score
719
Natafuta vijana wa kuniuzia juice fresh za matunda za kutembeza kwenye madumu
-wa kike /kiume
-Dumu la lita 5 akimaliza tatu kwa siku
-Mshahara 150,000/=
-Nauli natoa ya kwenda anapotembeza.
Alie tayari weka namba ntakupigia.
-Nipo Dar es salaam temeke
 
Natafuta vijana wa kuniuzia juice fresh za matunda za kutembeza kwenye madumu
-wa kike /kiume
-Dumu la lita 5 akimaliza tatu kwa siku
-Mshahara 150,000/=
-Nauli natoa ya kwenda anapotembeza.
Alie tayari weka namba ntakupigia.
Kamilisha Tangazo Lako, Upo Mkoa, Wilaya, Kijiji, Mtaa Gani
 
Halafu watu wanalalamika hakuna ajira; ingekuwa tangazo la ofisini watu 5000 wangekuwa wameleta maombi, ila la kutembeza juisi wanaweza wasipatikane.
 
Mbona kama sijaelewa hivi! Kijana akimaliza dumu 3 za lita 5 kwa siku ndiyo anapewa mshahara wa laki 1 na nusu!

Au atatakiwa kumaliza kila siku dumu 3 za lita 5, ndiyo mwisho wa mwezi analipwa huo mshahara wa shilingi laki 1 na nusu? Na asipotimiza hayo malengo uliyo muwekea, inakuwaje? Maana siyo kila siku ni Jumapili!!

Hebu unyooshe maelezo tafadhali.
 
Lazima uchague usiopokuwa mchaguzi kwenye maisha unaweza hata kuokota makopo na huku ni bachelor degree holder
Kama uhakika wa kula upo unaeza kuchagua, lakini kama huna uhakika wa kula mchana, utafanya kazi yoyote inayokuja usoni.
 
Utani huo ndugu kwa siku laki na nusu kweli tena juice??,huo ni mshahara kwa mwezi ndugu juice kubaki sio tatizo kwa siku moja moja lkn na sio kubaki dumu mbili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…