Natafuta wa kunisaidia mkopo

sexy bubble

Senior Member
Joined
Mar 29, 2014
Posts
156
Reaction score
22
Jamani nina shida kubwa sana, ndugu wameniandama hali hiyo inanifanya nijiskie vibaya sana. Ni wapi naweza pata mkopo wa shilingi laki mbili au tatu nirejeshe kwa mwezi au kama kuna mtu wa kuweza kunisaidia humu ndani naomba anisaidie naomba.

Kwa ambaye anaweza kunisaidia naomba ani pm nimuelezee shida niliyo nayo.Sijawa open kuekezea shida kwa wote kwa ajili ya usalama wangu.

Naomba jamani mimi ni mwaminifu siwezi fanya ujinga.

Asante kwa kusoma.
 
Kibo10 hebu msaidie bana, kwani hadi ujue jinsia?
DEMBA kuna jinsia zingine kama yako inaongezaga nguvu kwenye msaada
Hata mtu ukichoka ukiulizwa umechoka?"unasema"aah bado kabisa kumbe upo hoi balaa!
 
Last edited by a moderator:
Unajua mficha uchi hazai.
Wewe weka shida yako wazi.Unaweza kukuta mtu akakupa Buree bila hata kukudai.
Humu wote usituone hivi tuna madeni telee,lla tumo tu humu tunajifariji.Na ndio maana unaweza kukuta member anaingia humu yeye ni matusi mwanzo mwisho,yaani anahamisha tension za nyumbani analeta humu inakuwa sehem ya burudani.Na ndio maana Jf hakuna anaenuna labda awe wa Mkoani.
Watu wanamatatizo ya kifamilia humu wakikuambia utaona bora uzikwe,ila humu Jf ni sehem ya faraja,unaweza kukuta mtu anachangia mada ya mamilioni lakini anamadeni akiona sim inaita roho inadunda.
Huyu alieleta sim sijui nani,maana zamani anaekudai lazima aje,na ukimsikia mbio,ila siku hizi kazi kweli.Ugonjwa wa moyo umeongezeka kwa sim za tunaodawia.

Nakushauri weka wazi,Pesa sio utatuzi wa matataizo yako,unaweza kupewa ushauri ukawa ni bora kulikopesa,au ukakupa muongozo wa namna ya kulitatua.Unakuta wengi tunafikiria kwamba pesa ndio inatatua kila kitu,na ukiwa na dhana hii basi huto piga hatua,itakuwa wewe ni mchumia matatizo na unakwepa changamoto,na anaekwepa changamoto za kimaisha basi siku zote ni mtu wa huzuni.
Ni sawa na kuomba mkopo Bank bila ushauri wa kina,ukizipata hujui hata umefafanya nini,badala ya kutatua tatizo ndio unaongeza.

 
Ndugu yangu natamani sana ningeweka wazi yaliyo nisibu ila naogopa ndugu zangu watajua ukweli wa mambo.Humu jf wengi wanapitia na ndugu zangu pia ila hatujuani id kwa hiyo naogopa wasije waka gundua.Mimi najitajihidi niweze kutatua hali niliyokua nayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…