Natafuta wa kunizalia mtoto tu!!

JERUSALEM 2006

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2012
Posts
527
Reaction score
596
Habari wana jf;
Nina kaka yangu wa karibu sana ambaye anatafuta mwanamke atayekuwa tayari kumzalia mtoto.

Bro wangu huyu amehangaika sana, kila mwanamke anayempata hataki kuzaa naye kwani kaka anachotaka ni mtoto tu, halafu hakuna uhusiano utakao fuata baada ya hapo.

Yuko tayari kumlipa mdada au mmama yeyote atakayejitolea kuzaa naye, ila baada ya mtoto kufikisha miaka miwili atakua mali ya baba pekee na mama wa mtoto hatokua na haki yeyote kwa mtoto huyo.

Ni matumaini yangu wadada kwa wamama wa jf mtakua tayari kujitolea na kumzalia mtoto kaka yangu, kwani ameangaika sana jamani.

Kama uko tayari jus ni PM NAMBA YAKO YA SIMU AU E~MAIL THEN NITAKUTAFUTA.
asante
 
Kila la heri katika kutafuta hiyo mashine ya kutengenezea watoto.
 
Jamani jamani.Muwe mnaangalia na haki za watoto..Watoto nao wana haki ya kupata mapenzi ya baba na mama..Unamtaka mtoto peke yako umfanyaje!?wa kafara!?
 

Wewe na kaka yako mmechanganyikiwa. Kuoa hamtaki mnataka watoto! hovyooooooooooo
 
Isije ikawa mnataka mtoto wa kutoa kafara nyie au?? mbona sijawaelewa??
 
Kama amemkosa huko alipo hampati hapa jf akimpata me nahama mji
 
kamwambie umemkosa mwanamke huyo! halafu muulize kwanini hataki kuoa anataka mtoto asiye na mama tu????????
 

Wewe na kaka yako ni mataira. Binadam si mnyama kama kuku ama mbuzi kusema atapandikizwa hivo na ananunuliwa ki hivo.
Hiyo kusema mtoto ni haki ya baba tu ndio kwanza nasikia. Uwezi kumnyima binadam haki yake ya kuwa na mama. Laana tupu, na huyo atakae kubali ni taira pia.
 
Hiyo imekaa kibiashara zaidi...mbona hujatoa donge nono kwenye huo mkataba. Mtu hawezi zaa halafu akose haki za mtoto wake hivi hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…