Mkuu, kwanza hongera kwa kuwa na ujasiri wa kuingia kwenye sekta binafsi na kujiajiri mwenyewe. Hata hivyo nina swali moja? Hiyo Trademark yako (Dodoma Sunflower) imekuwa registered? na Je bidhaa zako zina nembo ya TBS? Kama jibu ni HAPANA basi yafanyie kazi hayo, na kama jibu ni NDIYO basi endelea kusoma hapa; Soko la bidhaa hizo zipo popote pale, kwani mafuta ni bidhaa inayotumika kila kukicha na pia haya ya Alizeti ni CHOLESTEROL FREE.
Cha kufanya ni kutafuta wenye maduka ya Jumla au taasisi zinazohudumia watu wengi (kama vyuoni, shule). Vilevile ninaweza nikakuunganisha na hawa wadau kama Jibu la maswali ya hapo juu litakuwa ni NDIYO
Changamoto kubwa niionayo mimi kwa watu wengi wanaokamua alizeti ni hapo kwenye MARKET SEGMENTATION. Unapoamua kupack kwenye vifungashio vya 5ltrs & 20ltrs ni vyema, lakini unakuwa umejitenga na soko kubwa zaidi la wale wanaomudu 1ltr & 3ltrs, kwani watanzania tulio wengi ni kima cha chini. (chukua hii kama changamoto na uifanyie kazi pia).