Natafuta watu wa kujitolea kwenye Taasisi isiyo ya Kiserikali (NGO)

Natafuta watu wa kujitolea kwenye Taasisi isiyo ya Kiserikali (NGO)

Joined
Aug 19, 2021
Posts
38
Reaction score
58
Habari Wananzonde jukwaani

Nimesajili shirika NGO mwaka 2020 ina usajili wa kufanya kazi mikoa yote Tanzania bara (Usajili wa kitaifa) lakini Hadi leo sijafanikiwa kupata fund Mahali popote .
Nimejifanyia tathmini nimegundua kwamba Sina watu wenye weledi kwenye hii NGO. Kwani 99% ya wanachama ni darasa la saba na hawaelewi Mambo ya NGO.

Maeneo ambayo nimefeli zaidi ni
1.Fund raising
2.Project guider
3.Mornitoring and evaluation
4.Project writing
5.IT and NGO branding


Ninaomba Kama Kuna mtu yeyote anaweza KUJITOLEA aje tufanye kazi.

Kwa kuwa hatuna fund kabisa sio lazima aje hapa nilipo ila Kuna kazi anaweza kuzifanya hukohuko aliko Kama issue ya branding, fund raising,project writing nk.

Pindi Hali ikitengamaa tunaweza ona namna ya kushirikiana kwa ukaribu zaidi

Shirika linajihusisha na child rights protection.
Kwa maelezo zaidi njoo watsap 0766432676.
 
Habari Terminator. Ungeandika maelezo ya ziada kupunguza maswali na sintofahamu. Huenda lengo lako ni jema la kutomchosha msomaji, ila nahakika unataka mtu wa kazi ambae atajitolea kihakika. Watu hao huwa hawachoki kusoma thread ndefu ambayo wanafahamu wanaeza kua msaada.

Andika wasifu wako kwa uchache watu wakufaham japo si kwa undani kihivyo.

Andika japo maelezo madogo ya hiyo NGO yako: Mission, Vision, Objectives, na location ya ofisi.

Andika idadi ya watu unaohitaji pamoja na majukumu ya kila mhusika kwenye nafasi yake. Namaanisha andika position (pamoja na number of volunteers needed) & duties za kila volunteer kwenye position husika.

Kufanya hivo itasaidia kupata watu sahihi na itapunguza upotezaji wa muda na gharama za kifedha.
 
Ndio anatafuta experty volunteer ili mkamshauri na kumsaidia what best for the NGO. Ningekuwa mtwara ningepigapiga hapo kwenye project writeup na M&E
Sawa sawa ngoja ajaze jaze nyama tuelewe vizuri..siku hiz napenda kaz za patnership zaid
 
Nimeku PM Mkuu, nipe hata hiyo monitoring and evaluation,sina experience ila nitajifunza tu kazi
 
Kwanini usiandije proposal kwenye haya mashirika ya marekani ukapata fund?
 
Back
Top Bottom