Natafuta watu watano wenye nia ya kweli ya kutaabika sasa ili tutanue baadaye inshallah

Natafuta watu watano wenye nia ya kweli ya kutaabika sasa ili tutanue baadaye inshallah

mkuu samaritan unajua nini hiyo ni namna ya uandishi ili kuvuta mashabiki ili nisiwe mbinafsi nitaruhusu amendment yoyote ile kikubwa kutengeneza pesa
 
Mkuu naamini una lengo zuri tu ni moja ya njia muhimu za kujikomboa kiuchumi katika dunia ya leo. Ndhani umeanza vizuri tu kwakuwa umeonesha nia ya kutaka kufanya jambo. Nadhani ulitaka watu 5 na kila mmoja atoe 1 M kasha ndio mjadili mnafanyaje,hapo kuna changamoto zake. Nadhani ungeweka maelezo kidogo haswa kwa kuzingatia viashiria kadhaa kama vile
1: Utambulisho wako; hapa unaeleza kidogo kuwa wewe ni kijana unayeituma, unataluma ya animal sciencw haswa kwenye mambo ya urutubishaji,ukuzaji na ufugaji wa wanyama kadhaa.(huu ni mfano tu). Then useme unapatikana wapi

2: Onesha wazo unalotaka kulifanyia kazi. Hapa unaweza sema kuwa ushaweka mchanganuo wa ufugaji wa kuku aina ya G4(kama mfano). Toa estimated cost kuwa ni around 5M. Hapa kwa kuhofia watu kuiba wazo sio lazima uweke mchanganua wako hapa ila wale ambao watakuwa tayari kufanya kazi na wewe hakuna namna ni lazima watapaswa kuupata.

3: Eleza aina ya watu unaohitaji kushirikiana nao na aina ya ushirikiano unaotaka. Mfano labda uatataka partners wawe na elimu ya biashara,mwingine sharia,mwengine project management na mwingine ICT. Hapa ni kama unataka ujuzi wa wanachama kuwa na mchango kwenye kuendeleza mradi. Ila pia sio lazima uanaweza kuwa na watu hata kama wote ni wa fani moja. Hoja kubwa hapa lazima wawe watu wanaojitambua,kujituma na ufahamu mzuri.

4: Eleza pia sehemu ambako kwa sasa unatarajia kufanya mradi. Hii itasaidia watu kujitathmini kama wanaweza kuwa sehemu ya mradi au la. Onesha pia kama unataka hao members kuwa ulipo wewe /(ndani ya mkoa ambako project inafanyika)

5: Eleza pia kama mtu hayopo huko na anapenda kushiriki atashiriki namna gani. Onesha namna ambavyo uaminifu utakuwepo kwani siku hizi kuna utapeli mwingi,kiasi kwaba hata wale wa kweli hawaaminiki tena. Weka wazi kuwa malipo yote yatafanyika kwa utaratibu maalumu baada ya watu kujiridhisha na pia yatapitia benki.

6: Eleza namna watu watakavokuwa wanawsiliana au kukutana. Kwakuwa hapa ni mambo ya fedha ni lazima mwishowe watu wafahamiane physically kwahiyo eleza utaratibu utakaotumika kuonana physically.

7: Karibisha mawazo na eleza tu kuwa kunanafasi ya kuboresha wazo hasa baada ya members kupatikana,kukubaliana na kuweka taratibu nzuri.

NB: Hayo unapaswa kuyaeleza hapa "Publicly" ili uweze kupata watu ambao ni kweli wamedhamiria kuunganisha nguvu. Sio rahisi ukawajibu watu kwenye PM kwa kiwango cha kutosheleza,na wengi kwenye PM hawatahangaika sana.Ila pia kuweka hayo maelezo hapo itaongeza imani kwa watu na kuonehsa usiriasnes wako. Naamini inawezekana na binafsi nakutia moyo katika hili. Kila la kheri brother..
 
Mi nadhan peke yangu sitoshi japo wazo langu ni kufanya project yoyote ile ambayo ni viable na zaidi itawagusa watu wa kati kwahiyo nikuondoe shaka nitalifanya hilo japo kwa ufupi ili nieleweke lkn tusiwaze sana pesa sabab pesa sio kitu static sana bali lengo langu tufanye kweli na sio maneno tu
 
Unajua watu wana jf wanatatizo moja la kujiona wao wakiwa na elimu fulani wamemaliza kila kitu kumbe sio ktk mafanikio yaan kuna muda mpaka darasa la saba wanahitajika ktk mchakato wa maendeleo mathalan tutaitaji shamba boy hiv utamuweka graduate pale bila anasa
 
Back
Top Bottom