Maadili ya Kiislamu ni yapi?
Sent using
Jamii Forums mobile app
Awe anasali sala tano kwani sala ni nguzo ya kwanza ili mtu awe muislamu na mtume amesema tofauti kati ya muislamu na asie muislamu ni sala
Awe msafi maana mtume Muhammad amesema Uislamu ni msafi basi jisafisheni
Awe anajihifadhi kulingana na maelekezo ya kiislamu kwani mtume amesema anamhakikishia pepo yule ambae atajihifadhi vilivyopo baina ya mapaja yake mawili
Awe anafunga mwezi mtukufu wa ramadhani kwani quran imesema funga ni faradhi kwa kila muumini ili apake kuwa mchamungu
Asiwe mlevi wala asiwe mzinifu nje ya ndoa maana quran imesema zinaa ni uchafu ulio mkubwa
Awe anahifadhi mwili wake kulingana na stara iliyoelekezwa na dini tukufu ya kiisalamu kama quran ilivyosema kuwa wanawake wateremshe nguozao zifunike vifua vyao na uchi wa mwanamke ni mwili mzima isipoluwa viganya vya mikono na uso
Awe anajua kusoma quran ata kwa juzuu ya amma na awe anaelimu maana mtume amesema kusoma ni lazima kwa kila aliye mwislamu na hawawezi kuwa sawa waliowasomi na wasiowasomi
Asiwe mshirikina kwani Mtume Muhammad s.a.w amesema uchawi ni miongoni mwa makosa saba yenye kuangamiza na kwa yeyote anaefanya ushirikina akifa atakuwa miongoni mwa watu wa moto mkali kabisa
Asiwe msengenyaji maana quran imesema kusengenya ni sawa na kula nyama ya ndugu yako aliefariki.
Awe anachunga ulimi wake maana mtume Muhammad amesema hajaacha jambo gumu kwa umma uliobaki kuweka kulikabili kama ulimi, akimaanisha zama hizi uongo, usengenyaji, fitina na utapeli umechupa mipaka
Kuna kitu hakijaeleweka?
Sent using
Jamii Forums mobile app