Natafute mke Muislamu

Natafute mke Muislamu

Is-haqqa

Member
Joined
Dec 12, 2019
Posts
28
Reaction score
46
Assalam alykum
Natafuta mwanamke wa kumuoa awe muislam ana maadili mazuri ya kiislam.
Umri wake kuanzia 23 hadi 30.
Mi ni mwislam umri wangu 30
Nimeajiriwa
Naishi Dar es salam
Aliekuwa tayari ambae yupo serios inbox me tufahamiane.
Narudia mwenza lazima awe muislamu
 
Maadili ya Kiislamu ni yapi?
 
Maadili ya Kiislamu ni yapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Awe anasali sala tano kwani sala ni nguzo ya kwanza ili mtu awe muislamu na mtume amesema tofauti kati ya muislamu na asie muislamu ni sala

Awe msafi maana mtume Muhammad amesema Uislamu ni msafi basi jisafisheni

Awe anajihifadhi kulingana na maelekezo ya kiislamu kwani mtume amesema anamhakikishia pepo yule ambae atajihifadhi vilivyopo baina ya mapaja yake mawili

Awe anafunga mwezi mtukufu wa ramadhani kwani quran imesema funga ni faradhi kwa kila muumini ili apake kuwa mchamungu

Asiwe mlevi wala asiwe mzinifu nje ya ndoa maana quran imesema zinaa ni uchafu ulio mkubwa

Awe anahifadhi mwili wake kulingana na stara iliyoelekezwa na dini tukufu ya kiisalamu kama quran ilivyosema kuwa wanawake wateremshe nguozao zifunike vifua vyao na uchi wa mwanamke ni mwili mzima isipoluwa viganya vya mikono na uso

Awe anajua kusoma quran ata kwa juzuu ya amma na awe anaelimu maana mtume amesema kusoma ni lazima kwa kila aliye mwislamu na hawawezi kuwa sawa waliowasomi na wasiowasomi

Asiwe mshirikina kwani Mtume Muhammad s.a.w amesema uchawi ni miongoni mwa makosa saba yenye kuangamiza na kwa yeyote anaefanya ushirikina akifa atakuwa miongoni mwa watu wa moto mkali kabisa

Asiwe msengenyaji maana quran imesema kusengenya ni sawa na kula nyama ya ndugu yako aliefariki.

Awe anachunga ulimi wake maana mtume Muhammad amesema hajaacha jambo gumu kwa umma uliobaki kuweka kulikabili kama ulimi, akimaanisha zama hizi uongo, usengenyaji, fitina na utapeli umechupa mipaka

Kuna kitu hakijaeleweka?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Assalam alykum
Natafuta mwanamke wa kumuoa awe muislam ana maadili mazuri ya kiislam.
Umri wake kuanzia 23 hadi 30.
Mi ni mwislam umri wangu 30
Nimeajiriwa
Naishi Dar es salam
Aliekuwa tayari ambae yupo serios inbox me tufahamiane.
Narudia mwenza lazima
unataka mke kweli ???au unatafuta msichana mtakae dumu ktk mahusiano kisha ndoa
 
Yupo mdada namfaham ana hizo sifa anatafuta nusra ila single mother vipi nikuunganishe nae. Ana watoto wanne ila dini masha-Allah hadi nikabu anavaa.
 
Back
Top Bottom