Nataka kadi ya CCM rasmi

Nataka kadi ya CCM rasmi

Nduka

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2008
Posts
8,553
Reaction score
2,380
Najua mtanishangaa lakini nimepata ufunuo kuwa mabadiliko ya haraka yatawezekana iwapo tu nguvu hiyo inatoka CCM(sijasema hayawezekani ila nimesema ya haraka). Kwa wanaofuatilia muelekeo wa siasa za nchi hii nguvu hii ya mabadiliko imekwisha anza kujidhihirisha, matukio ndani ya chama na kwenye serikali yanatoa taswira ya mafanikio muda si mrefu cha msingi ni kuongeza nguvu ndio maana nimekata shauri nachukua kadi. Siri za vyama vya upinzani zilizo mezani(za kufadhiriwa na CCM) na zilizo gizani ni dalili ya kuendelea kuchoshana tu huku watu wetu wanaendelea kuteseka kwa njaa,umasikini, kukosa elimu bora, huduma bora za afya na mateso yanayotokana na CCM hovyo, siwezi kusubiri vyama vya upinzani vibadilike huku nikishuhudia hayo nawafuata akina NAPE,JERRY na vijana wengine machachari tuinyoroshe CCM.
Nani yupo pamoja nami???????
 
Burn,

tatizo si kuwa na kadi ya CCM na kujiunga na Kina Slaa,Je utakisaidia vipi CHAMA na Nchi yako kwa ujumla?

karibu CCM ya Vichwa ambo wana uwezo wa kuwakemea wengine!
 
Burn,

tatizo si kuwa na kadi ya CMM na kujiunga na Kina Slaa,Je utakisaidia vipi CHAMa?

karibu CCM
 
Najua mtanishangaa lakini nimepata ufunuo kuwa mabadiliko ya haraka yatawezekana iwapo tu nguvu hiyo inatoka CCM(sijasema hayawezekani ila nimesema ya haraka). Kwa wanaofuatilia muelekeo wa siasa za nchi hii nguvu hii ya mabadiliko imekwisha anza kujidhihirisha, matukio ndani ya chama na kwenye serikali yanatoa taswira ya mafanikio muda si mrefu cha msingi ni kuongeza nguvu ndio maana nimekata shauri nachukua kadi. Siri za vyama vya upinzani zilizo mezani(za kufadhiriwa na CCM) na zilizo gizani ni dalili ya kuendelea kuchoshana tu huku watu wetu wanaendelea kuteseka kwa njaa,umasikini, kukosa elimu bora, huduma bora za afya na mateso yanayotokana na CCM hovyo, siwezi kusubiri vyama vya upinzani vibadilike huku nikishuhudia hayo nawafuata akina NAPE,JERRY na vijana wengine machachari tuinyoroshe CCM.
Nani yupo pamoja nami???????
Nipo pamoja nawe kama usemi wako ni dhahiri,ila wasiwasi wangu ni kuwa ukishalambishwa halua utanywea,ila kama wewe ni ngangari alutacontinua.
 
Chama Cha Majambazi na Mafisadi, CCM Stinks !!
 
That's democracy. Una haki ya kujiunga na chama chochote mkuu bila hata kufafanua au kutolea maelezo maamuzi yako. Najua siyo wanaCCM wote walio wachafu na siyo upinzani wote uliyo safi. WHich ever party you go to it is democracy at work.
 
Chama Cha Majambazi na Mafisadi, CCM Stinks !!

Greeque atleast hapo tayari tunajua tatizo, na malengo ni kubadilisha na nina uhakika tutafanikiwa, huku pengine hata hayo uliyosema hayaonekani.
 
Greeque atleast hapo tayari tunajua tatizo, na malengo ni kubadilisha na nina uhakika tutafanikiwa, huku pengine hata hayo uliyosema hayaonekani.

Kwa hiyo Mazee Burn unategemea utaenda kukisafisha Chama kutoka kwa Mapapa na Manyangumi ya Ufisadi, angalia tu wasije wakakubadilisha.
 
Burn,

tatizo si kuwa na kadi ya CMM na kujiunga na Kina Slaa,Je utakisaidia vipi CHAMa?

karibu CCM

Ndugu yangu najua mimi si malaika lakini nitahakikisha kipindi chote nitakacho kuwa katika chama katika ngazi yoyote ile, misingi ya TANU ya haki na usawa inarudishwa.
 
Wenye akili tuliisha mjua huyu bingwa....kila laheri msalimie Makamba! kwanza hukuhitaji matalumbeta wewe nenda tu, watu wengine bana!
 
Nataka kadi ya ccm rasmi
Jamani huyu anataka kadi ya CCM rasmi, maana ameona CCM ya sasa hivi si rasmi. Niliwahi kusikia kuwa kuna CCM mtandao, CCM Asili, etc na sasa Burn amekuja na CCM Rasmi.
 
Kwa hiyo Mazee Burn unategemea utaenda kukisafisha Chama kutoka kwa Mapapa na Manyangumi ya Ufisadi, angalia tu wasije wakakubadilisha.

Kunibadilisha hawatoweza mkuu kwani nguvu yao imefikia ukingoni nadhani dalili zao kutapatapa umekwisha ziona, marekebisho kidogo siendi kukisafisha chama bali naenda kuongeza nguvu katika wimbi la mabadiliko huko mzee,cha kufurahisha zaidi watu safi CCM ni wengi zaidi ya hao waliochafuka suala ni kuwakumbusha tu hao walio wengi kuwa wao ndio nguvu ya chama licha ya ufukara wao.
 
Greeque atleast hapo tayari tunajua tatizo, na malengo ni kubadilisha na nina uhakika tutafanikiwa, huku pengine hata hayo uliyosema hayaonekani.

Hofu yangu ni wewe kubadilishwa badala ya kukibadilisha chama na wanachama
 
Hofu yangu ni wewe kubadilishwa badala ya kukibadilisha chama na wanachama

Kweli ndugu yangu kuna hatari kama hizo, lakini nashukuru kuna wakuu zangu kama wewe na pia wapo watu safi huko wataninyoosha pale nitakapo pinda.
 
Mmmh! aisifuye mvua basi imemnyeshea.....walikuwa wapi siku zote?
siko pamoja nawe.
 
Mmmh! aisifuye mvua basi imemnyeshea.....walikuwa wapi siku zote?
siko pamoja nawe.

Nakubali kutokukubaliana na wewe mkuu japo sijajua msimamo wako, vipi mwenzangu wewe ni Chama gani?
 
bwana burn ni wewe ndo mheshimiwa Lwakatare au? maana tuliambiwa ataingi ukumbini.. karibu.. lkn la kushangaza nahisi tayari jamaa washakubadilisha kabla ya wewe kuwabadilisha maana tumezowea kuona kina Tambwe,Salum msabah,Kabouru,Lamwai wakibadilishwa halafu ndo wanajiunga na CCM RASMI.. wakowapi? hongera Kwa mafisadi kukunua..
 
Back
Top Bottom