Mpita Njia
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 6,997
- 1,172
Simpo, ukijiunga upinzani sasa hivi utakuwa na kazi ya kuwabadilisha. Ukishafanikiwa kuwabadilisha utakuwa na kazi nyingine ya kuibadilisha CCM. Utakuwa umezunguka sana na kuifanya kazi maba 2. Ukijimwaga CCM moja kwa moja unakuwa na zi moja tu, kuwabadilisha wao, kwishaKwa nini usubiri vibadilike na usiungane nao kuwabadilisha na badala yake unajiunga na CCM unayoita ovyo kuibadilisha. Unasema unawafuata NAPE, JERRY na vijana wengine machachari - hawa wamefanikiwa nini cha kujivunia ndani ya CCM.
Ahsante sana mkuu natumaini na wewe ni mmoja wetu sisi tunaokerwa na hali ya nchi yetu kwa sasa, ndio maana sikutaka kuwajibu wale walio hoji mimi ni nani hadi nikajipa uwezo wa kuibadilisha CCM, wewe ni jibu la uwezo huo kwani naamini ndani na nje ya CCM kuna pundamilia07 wa kutosha kubadili hali ya sasa.Mungu ibariki Tanzania ..Kidumu CHAMA CHA MAPINDUZIBurn,
I support and respect your decision. Tunahitaji watu ambao wanakiu kabisa ya maendeleo ya nchi hii kama wewe ambao wako tayari kuthubutu kugeuza mawazo yao kuwa vitendo.
CCM ni chama kikubwa na chenye mtandao mpana wenye wanachama wengi. Kinachotakiwa ni kuhakikisha unakuwa innovative, unajituma vya kutosha, unajenga uhimili wa kutoa ushauri katika ngazi mbali mbali za chama hasa baada ya kufanya researches za kutosha. Kwa vile utakuwa unaingia katika kundi jipya kwako, apply the scientific proven abc steps in forming a workable group ambazo ni Forming, Storming, Norming and Performing. Yeyote anayekwenda CCM kwa malengo ya kuwatumikia wananchi ana nafasi kubwa ya kuwafikia na mchango wake kuwanufaisha walengwa.
Hujachelewa!!!!!
Si kweli hata kidogo kuwa CCM ni chafu na inahitaji mabadiliko makubwa hasa kwa watu wasio na vision ya uelewa hali halisi ya nchi yetu na matokeo yake umeinarrow fikra yako kwa kiwango cha ajabu .QUOTE]
Hapo ndipo tunapishana mzee, mimi nafikiri kwa zaidi ya miaka arobaini chama kimeshindwa kuwaongoza watu kwenye maendeleo, ushahidi unaonesha wazi kuwa pamoja na vijihatua vidogo kuelekea kwenye maendeleo bado kundi kubwa la watanzania ni masikini na hizi hazikuwa ni fikra zilizoijenga CCM hapo awali..nadhani kwangu hilo ni tatizo kubwa. Hayo mengine ya kudai sijui wa tz ni wavivu ni sehemu tu ya kizazi cha CCM kutaka kukwepa majukumu, kuna tatizo la sera huwezi kutegemea nchi kuondokana na umasikini kwa watu wake kuuza baa kwa bidii.
baki huku huku kwa kuandika kama unaona ndio ukombozi kwako, maana kama huna chama andika kuwa mgombea binafsi