Nataka kuacha kazi niwe mjasiriamali, naombeni ushauri

naliwe

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2013
Posts
410
Reaction score
987
Nina miaka sita toka niajiriwe kwenye kampuni flani,
Mshahara wangu ni tsh 800000 kwa mwezi ambao ukikatwa na makato pamoja na marejesho ya mkopo napokea tsh 421000 kwa mwezi

Familia yangu ni ya watu watatu yani mama,baba,na mtoto mmoja

Nimebahatika kununua Noah mbili ambazo nazifanyia biashara kila moja inanipatia tsh 40000 kwa siku ni sawa na 80000 kwa noah zote mbili

Kwa mwezi ni sawa na 2400000,kiasi ambacho ni Mara tatu ya basic ya mshahara wangu

Nina leseni ya udereva na wakati mwingine naendesha mwenyewe,

Sasa nataka niache kazi ya kuajiriwa ili nijikite zaidi kwenye biashara maana naona inalipa zaidi

Naombeni ushauri
 
Usichezee kazi hizo Noah zimetoka kwenye kazi hiyo hiyo utateseka ndugu yangu.Kwanza ukiacha kazi ibirisi jinsi asivyokuwa na hodi hizo Noah zikikamatwa Mara 2 kwa wiki na na trafiki ukalipa faini yao hapo ndiyo utaanza kukumbuka kazi na majuto atakuwa mjukuu.
 
Halafu kazi yenyewe ukute ndo uticha...!!!
Hapo sihitaji ushauri aisee ni kama safari ya kuhama nchi hii yani sitafuti ushauri kwa mtu nikipata nafasi hiyo.
Fastaaaa..!!
Bwaga kamanda,kuajiriwa ndo mwisho wa akili zako hapo.!!
 

Mkuu, jipangie malengo yaani miaka 3 hadi 5 mbele halafu utaangalia unataka kufanya nini.

Ila endelea na ajira yako na ziachie Noah zikuingize pesa kama miaka 3 au 5 hivi.

Baada ya hapo utaangalia upanue biashara hiyo au uanzishe biashara ingine.

Kwa mfano kama una nyumba ambayo ndiyo ya familia basi ongeza ingine uipangishe.

Pia anza ufugaji wa kisasa au ukulima wa kisasa yaani unanunua mashine ya kulimia ya kuvuna na unakuwa ukizikodisha.

Hivi vijimradi vidogovidogo vitakusaidia kufanya majumuisho ya mapato yako kwa mwezi na kwa mwaka.

Wakati unafanya haya yote ndiyo unajiandaa kuacha hiyo kazi yako.

Hivyo nakushauri uache kazi baada ya miaka 5 kuanzia sasa.
 
Nimecheka sana kwenye hii mada....... hofu hofu hofu. Ukiwa mwoga hutokaa uendeleee

Biashara ya nyumba ya kupangisha hailipi..... Msimdanganye (jenga kwa lengo jingine sio kupangisha kama biashara) ukitaka kama biashara basi kajenge obay, masaki etc au jengo lodge/guest/hotel

Kubwa kabla ya kuacha kazi jiulize unataka kufanya nini? unauzoefu nacho?


Nina miaka 10 sijawahi kuomba ama kuandika barua ya kuomba kazi
 
Sasa ndugu yangu umesema umepata hizo gari Noah kwa ajili ya kazi kwa maan umepata mkopo wa kununulia .

Sasa ukiwacha kazi uwoni utakuwa na mzigo mwingine wa kulipa Deni ambazo zitatoka Direct ktk kipata hicho cha Noah

Je ungekuwa huna kazi ungepata hizo Noah ?
 

Mkuu, jamaa ana mkopo hivyo si mbaya kama akijipa muda amalize mkopo.
 
Nilichokiona humu ni woga wa maisha! Ukitaka kugombana na familia,ndugu waambie una mpango wa kuacha kazi! Mtu analipwa 800,000 kuna buashara inamuingizia 2.4m anataka kuacha kazi asimamie mwenyewe hio biashara watu wanamwambia asiache kazi.

naliwe kama moyo wako na akili yako inaamini unachotaka kufanya acha kazi. Ukisikiliza ushauri hutafanya chochote. Kukuongezea tu hio Noah ukiendesha mwenyewe kwa siku utapata mara mbili ya anayokuletea dereva na gari itadumu zaidi.

Siri ya biashara ndogo nndogo hizi ni kusimamia mwenyewe na ukiwa na discipline ya maisha lazima ufanikiwe.
 
Wakuu hivi mfanyakazi wa serikali anaruhusiwa kufanya biashara...Kama Ndiyo Ni kwa Sheria ipi
 
Nakushauri uendelee na kujiwekeza lakini tumia kazi kama sehem ya kukopa yaani kila unapomaliza deni unakopa na ukiwa akilini mwako unajua kua kipato chako kipo kwenye pale umewekeza. Usiache kazi ndg we piga kazi wakati unaelekeza nguvu nyingi kwenye uwekezaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…