Nataka kuacha kazi niwe mjasiriamali, naombeni ushauri

Nataka kuacha kazi niwe mjasiriamali, naombeni ushauri

Mkuu jilipue usisikilize ushauri wa viumbe waitwao wanadamu. Watakukatisha tamaa bure. Ukikubali kuajiriwa ukubali pia kuwa mtu wa kipato cha kujikimu. Yaani ule,uishi na uvae pamoja na kusindikiza umri.
 
Watanzania tulio wengi tunahofu ya kuacha kazi tunapokuwa nayo kwa sababu ya hofu ya maisha ya baadaye...Hujawahi kujiuliza kwanini biashara nyingi na viwanda ni vya wageni hasa Wahindi na wachina...Naungana na Kagame..matatizo yetu weusi mengi tumesababisha wenyewe..Nothing is easy
 
Haloo acha kazi ukiendelea mwisho utakua maskini,Mimi niliacha kazi tangu mwaka Jana kwa utoro kazini,lakini nilijipanga na kufanikiwa kulima heka kumi na kuvuna viroba 117 nilikuja kuuza mpunga huo 100000/kwa kila kiroba. niliuza roba 100 ni sawa na tsh 10000000/ nikaanza biashara hadi sasa ninakaribia kua na mtaji wa million 70 aisee niligundua kua ningebaki utumishi ningeambukia ka sarrary tu.na sitarajii kuajiriwa tena. Na nimeajiri vijana wa 5 na nawalipa350000 kwa mwezi,hapo mkuu jiongeze kama ni muoga wa maisha baki uko.
 
Nina miaka sita toka niajiriwe kwenye kampuni flani,
Mshahara wangu ni tsh 800000 kwa mwezi ambao ukikatwa na makato pamoja na marejesho ya mkopo napokea tsh 421000 kwa mwezi

Familia yangu ni ya watu watatu yani mama,baba,na mtoto mmoja

Nimebahatika kununua Noah mbili ambazo nazifanyia biashara kila moja inanipatia tsh 40000 kwa siku ni sawa na 80000 kwa noah zote mbili

Kwa mwezi ni sawa na 2400000,kiasi ambacho ni Mara tatu ya basic ya mshahara wangu

Nina leseni ya udereva na wakati mwingine naendesha mwenyewe,

Sasa nataka niache kazi ya kuajiriwa ili nijikite zaidi kwenye biashara maana naona inalipa zaidi

Naombeni ushauri
Endelea kuongeza vitega uchumi,pale utakoona umeimarika zaidi kiuchumi ndipo uangalie pakwenda
 
Back
Top Bottom