Nataka kuachana nae ingawa bado nampenda

MR SILENCE

Member
Joined
May 20, 2012
Posts
13
Reaction score
2
Helo mimi ni mwanaume wa miaka 28 nina mchumba wa miaka 21 ambaye nimedumu nae kwa miaka miwili,juzi alinieleza kuwa baba yake hapendi aolewe na mtu wa kabila langu.Nilipotaka kujua msimamo wake hakutaka kusema chochote na mpaka sasa hayuko tayari kuzungumzia chochote kuhusu jambo hili akidai baba yake alikuwa anatania(hakuwa serious) pia imenikatisha tamaa kuendelea kumpenda maana hata kama atakuwa na msimamo tayari baba yake hata kuwa na amani kutupa baraka zake.Nimeogopa kumwacha sasa maana yuko chuo anafanya mitihani wiki hii ila baada ya hapo chochote chaweza tokea.Ukweli ni kwamba nampenda sana na sijawahi hata siku moja kumsaliti na sina mwingine zaidi yake.
 
Mmmh, mbona umri wako unatosha kabisa kufanya maamuzi?

Yaani mtu unamzidi miaka 7 naye akushinde kuongoza? Je familia utaweza.

Acha kuishi kitamthilia bana.
 
Ni mwanamke wangu wa kwanza sijawahi kuwa na mwingine kabla kiasi cha kujiona mgeni wa mapenzi
 

Chief, hapo kwenye bold amesema baba yake alikuwa anatania, sasa hofu ya nini?! Kwenye maisha utaishi na yeye au babaake? Kikubwa ni msimamo wake yeye binafsi. Inawezekana alikuwa anataka kukupima aone reaction yako na utayari wako kupambana na difficult situation kama hizo. Ila kama bado una wasi wasi na upendo wake kwako subiri amalize mitihani umuite akueleze msimamo wako ili usije ukawa unaweza kwenye mradi usiolipa!
 
Mkuu si ameishakwambia alikuwa anatania, sasa usichoelewa nini au hutaki utani?
 
Mmmh, mbona umri wako unatosha kabisa kufanya maamuzi?

Yaani mtu unamzidi miaka 7 naye akushinde kuongoza? Je familia utaweza.

Acha kuishi kitamthilia bana.

Dah! Exacly mamacita Kongosho - kama challenge hizi zinamshinda hakuna ndoa ataweza himili huyu...yani hendi kokote akioa.
 
Last edited by a moderator:
Wewe kabila gani na yeye kabila gani weka wazi upate msaada
 
Pardon please. . .

Kwa hiyo 21yrs anakufundisha a e i o u?
:lie🙁Basi mwambie hivi, unampenda sana, huwezi kumwacha hata mlima kilimnjaro uhamie Singida) basi hatamskiliza baba yake kuhusu kuachana


Ni mwanamke wangu wa kwanza sijawahi kuwa na mwingine kabla kiasi cha kujiona mgeni wa mapenzi
 
Yaani mie mimba ilikuwa na boyifurendi tena mtoto wa kihindi walikuwa majirani alipozaliwa akaitwa rejesh

Safi sana... umeanza mapenzi na 27yrs..Kumbe watu kama nyie bado mpo..ndio maana angalau tunapata mvua.
Akina Kongosho wameanza wakiwa na 6yrs!!
 
Kaka kabila langu la nini kwani tunataka kutambika au kazi ya Nyerere bado tumeisahau?
 
kama yupo chuo huyo ashapata kijamaa kingine ndio wanafanyiana mambo mpaka ameshaanza kukusahau, nyamaza kimya kamanda piga moyo konde, tulia atakuja maalum kwa ajili yako
 
Kwani wewe hujawahi ona ndoa zilizoanza kwa wawili kutoroshana na baada ya kuweka sawa zinadumu?????????Hapo nafasi ya wazazi ipo wapi???????Sema na Moyo wako juu ya mapenzi yako kwa Binti na sio Matakwa ya wengine ambao hawataishi na wewe
 
Jambo ni dogo sana halistahili uamuzi wa kuachana time will tell vumilia utakuja kujua kama baba alikuwa anatania au la au yeye alibuni sababu.
 
Baba yake analipenda sana kabila langu,kama vipi niunganishie mimi huyo mtoto nikusaidie kuoa,alafu kitakachofuata akubaliane na tabia zangu za ulevi sugu,kipigo na kushea penzi na mabaa maid coz nipo addicted nao sana,hapo ndipo atakapo ona umuhimu wa hisia au kabila katika ndoa.Swali linakuja kwako,kwani ulimtongoza baba yake au yeye,na je ulipomtongoza alimuambia baba yake kama katongozwa?na kama alimuambia alikubaliwa kuwa na wewe?huyo binti keshapata sharobaro anamsumbua anakosa tuu namna ya kuachana na wewe!!But thats my take!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…