MR SILENCE
Member
- May 20, 2012
- 13
- 2
Helo mimi ni mwanaume wa miaka 28 nina mchumba wa miaka 21 ambaye nimedumu nae kwa miaka miwili,juzi alinieleza kuwa baba yake hapendi aolewe na mtu wa kabila langu.Nilipotaka kujua msimamo wake hakutaka kusema chochote na mpaka sasa hayuko tayari kuzungumzia chochote kuhusu jambo hili akidai baba yake alikuwa anatania(hakuwa serious) pia imenikatisha tamaa kuendelea kumpenda maana hata kama atakuwa na msimamo tayari baba yake hata kuwa na amani kutupa baraka zake.Nimeogopa kumwacha sasa maana yuko chuo anafanya mitihani wiki hii ila baada ya hapo chochote chaweza tokea.Ukweli ni kwamba nampenda sana na sijawahi hata siku moja kumsaliti na sina mwingine zaidi yake.