Fisadi.Jones
Senior Member
- Aug 15, 2008
- 110
- 7
Mzee hy 980 ni fob au cif price? kama ni fob price jumlisha na freight dola 800 +Jaai inspection usd 300 + insurance usd 50. total usd 2080. hy ni bei ya kuleta hl gari mpaka bandarini. then baada ya hapo tayarisha karibia ml 2.5 kwa ajili ya ushuru na charge nyingn pa1 na registration. km unalitaka ninaweza kukusaidia kuimport.
1. Minimum hii gari ita-cost US$ 2,300 CIF Dar (FOB=980, JAII=250, Freight=1000, Insurance = 50)
2. Exchange rate ya TZS 1,300 ni sawa na madafu TZS 2,990,000
3. Ongeza Import charge 25%, VAT ya 18%, port charges etc (make it 50% 0f the CIF value) inakuja [TZS 2,990,000 times 1.5 = TZS 4,485,000]
4. Kwa kuwa ni over 10 years old kuna charge ya 25% scrap tax
5. Then from (4) above, TZS 2,990,000 times 1.75 = TZS 5,232,500
6. Estimated clearing costs, registration costs etc kama minimum TZS 800,000
7. The total cost minimun is TZS 6,000,000 (unakiendesha mtaani)
Do!
Asanteni sana mzee dully na wengineo.
Sasa namnahii kweli tutaweza kuepuka kugombania daladala?
Mimi nikajua kwa kuchagua ka gari cha bei nafuu basi nikizichanga na kufika 3,000,000 hivi pengine ningeaanza ku-enjoy kwenda kazini.
Lakini invyoonekana itabidi nianze kunyanyua vyuma tu. Hiyo hela nitumie kula vyakula vizuri vya kujenga mwili.
Au mnashaurije wazee?
Marekebisho kidogo......ushuru wa uchakavu (scrap tax) ni 20% sio 25% mkubwa! kwingine kote tupo pamoja!
Amesahau Excise Duty ya 5% ya CIF+VAT+Import+Scap Tax. In total tax anayotakiwa kulipa ni 85.85% ya CIF. Halafu weka Wharfage ya 1.6% + VAT = 1.89% ya CIF, na Processing Fee (IDF) 1.2% ya CIF + $10. Bado gharama za agent, normally Shs 150,000 to Shs 180,000 plus registration fees.
Sio mbaya,ila pia bongo wapo wanaohitaji kubadilisha ladha ya magari. Unaweza ukapata za mtaani hapa hapa bongo badala ya kuagiza toka nje. Kuna watu kibao humu mtaani wanauza gari zao,onesha nia watakupa gari kwa hela hiyo au ongeza kidogo tu utapata gari bro.
Bei za gari zinazouzwa humu si unazionaga mzee? Yaani mtu anataja mil 12 kama vile ni chenji ya shopping ... lol ... sasa si tukitaja vihela vyetu si tutachekwa?
Kwa maeelzo niliyoyasuma huku, ukiona mtu anauza gari chini ya 5M basi ina matatizo. Ndio maana nkasema ngoja nijaribu kuagiza hata cha zamaniiiii cha bei ya chini kabisa. Nako pia naona si kwangu ... huu umasikini ndio ushatuganda wengine ....
Kwa data nilizozisoma hapa ni kwamba ili gari inigharimu 3,000,000 tu inabidi CIF iwe si zaidi ya $1,370. Je, wataalamu wa kukokotoa mnaweza kunihakikishia hili ili niwe ninasaka katika range hiyo tu?
Mkuu nakushauri ununue pikipiki tu ya Bajaj hutakaa kwenye foleni wewe ni kupenya tu na ni gharama nafuu kuiendesha kuliko gari. Kuna watu wana magari wanaendesha week end tu.
Mkuu gari yenye CIF US$ 1,370...mpaka unaiendesha itakugharimu kitu kama TZS 4,000,000....Hapo tayari upo barabarani mkuu!