Mkuu Fisadi mimi ninakushauri hivi kweli unaweza ukapata gari from Japan kwa hela uliyonayo il vitu vya kufikiri:
Uimara wa gari, jee inamiliki mikiki ya barabara za Bongo? waweza nunua gari isidumu hata miezi 6.
Kwa ushauri wangu bora zidundulize alau zifike millioni 5 waweza kupata usafiri wa maana tena hapohapo Bongo.
Ama kama una mtu UK muagizie Suzuki Vitara, hazina bei, ni imara na ukibahatika kwa millioni 5 waweza kusukuma huu mkweche Dar. Naongea kwa uhakika kwa vile kuna jamaa yangu ameshawahi kuleta hio gari na ilimgharimu millioni 5.
mfano hii hapa:
http://cgi.ebay.co.uk/1997-SUZUKI-V...s_UK?hash=item439a4c6a23&_trksid=p3286.c0.m14
Kwa pesa ya madafu utaipata kwa mill 1.8 maximum. ila waingereza ni watu wa kusikiliza best offer kama unampa huyu bwana £750 sawa na sh. mill 1.5 anakuachia mkweche. Freight mpaka Dar mill 1.5. kwa hio mill 3 kitu iko bongo, mazagaa mengine ya ushuru n.k
weka mpaka mill 2.5 jumla millioni 5.5 gari iko mitaani.