Nataka kuagiza gari kwa njia ya mtandao

Nataka kuagiza gari kwa njia ya mtandao

Wanajamiiforums wote mliochangia,nawashukuruni sana kwa ushauri wenu..
Ila kama kuna kurisk fulani hivi.
si unajua tena washikaji kaela kenyewe changama.

shukrani
 
kwa kweli sasa hv hali ya biashara kwa ku2mia mitandao imekuwa na wizi mkubwa. mfano katika hy tradecarview kuna blacklist ya makampuni ambayo yamefungiwa kwa kuchukua pesa kisha hawatumi magari. na wengi wa walioibiwa na watanzania. ila cha kushangaza makampuni hayo hayo yamebadili majina kisha yakasajiliwa tena. mfn kampuni ya prosper huyu jamaa mkenya ila yupo japan wanaongoza sana kwa kulalamikiwa kwa vitendo vya kuwauzia wa2 magari tofauti na wanayowaonyesha kweny picha. we have 2 be carefu guys

nimeshtuka sana nilipoona jina la prosper

huyo prosper ni hatari sana alikuwa anawatumia watu magari UK, anawaonyesha kwenye picha gari zuri, gari likifika ndani ni nyanganyanga na pia vitu kama bearings na mazagazaga kibao inabidi ubadilishe.
mimi ni mmoja wapo amabe niliuziwa gari na jamaa kupitia rafiki yake ninaemwamini. kutokea siku hiyo sijawahi kuagiza gari kutoka kwake tena na watu wa UK, kila mtu aliyeagiza gari mara ya kwanza ajarudi tena
beware
 
nimetumia japanesevehicles.com wako powa sana.

Mimi pia. They are so friendly na wana good quality cars. Wakati natuma pesa gari niliyokuwa nimeichagua ikawa imeuzwa wakanipa nyingine nzuri zaidi at a cheap price na kwa vile nilikuwa nimeshatuma pesa tayari, balance wakanirudishia. Gari ni ya mwaka 1999 na niliinunua mwaka juzi mpaka leo sijawahi kwenda gereji ni kumwaga oil tu na kubadilisha filter after 3000 km basi.

Hili ni kampuni la kueleweka na la uhakika 100 %.
 
Nataka kuagiza gari kwa njia ya mtandao je mtandao gani ni salama?

Je kuna mtu ameshawahii kuagiza kupitia mitandao hii,naomba msaada wenu

Je www.tradecarview.com na www.japantradecar.com hii vipi?

Nshukuru kwa msaada wenu

Binafsi sijawahi kuagiza kupitia mitandao, ila nina rafiki zangu walishaagiza na nitakupa mifano michache:

-Kuna walioagiza wakapata walichoagiza, nikimaanisha waliona gari mtandaoni, wakamaliza taratibu zote na wakatumiwa Gari lile lile waliloagiza kwa gharama zile zile zilizotajwa mtandaoni.

-Kuna mmoja aliagiza kufanya taratibu zote za malipo. In the end akaambiwa Gari aliyochagua wanasikitika iliuzwa kabla hajakamilisha taratibu za malipo (Lugha za biashara). Hata hivyo, wakaahidi kumtafutia Similar type. Ilichukua muda kidogo, wakapata Gari japo haikuwa choice ya mteja, (Of course wana update na kutuma pics za Gari wanazopata kwa mtu kufanya choice upya). SO finally akapata Gari, hakutakiwa kuongeza pesa yoyote cause walisema gharama ni sawa na Gari aliyoiagiza mwanzo (Alikuwa na bahati), though Tofauti iliyokuwepa kwa Gari aliyochangua 2nd time, ilikuwa KUBWA sana kulinganisha na Gari aliyochagua mwanzo. Anyway, alipata Gari, same make kwa same price.

-The worse one ni mmoja (Mpaka sasa anasubiri Gari/Refund). Aliagiza gari sometimes in July 2009. Akafanya taratibu zoote za malipo, in the end akaambiwa kama huyo wa pili. Of course aliambiwa aendelee kuchangua kwenye site na vile vile wao wakawa wanamtumia pics za magari waliyoyapata. Well, alibahatika kupata similar Car, na akaomba atumiwe hiyo, Guess what happened? Aliambiwa aongeze pesa kwani zile alizotuma hazifikii/hazitoshi kununua hilo gari alilochagua. Ila kwa yale wanayopata wao (Ambayo mteja hajaridhika nayo), wanadai bei ni sawa na ile aliyotuma kwa Gari ya mwanzo iliyouzwa! Hivi ninavyoandika bado wanaendelea kumtafutia Gari na mbaya hawataki kurudisha pesa! Matumaini yapo vile wanawasiliana.

Ushauri: Unaweza agiza na ukawa na bahati ya kupata kile ulichokichagua mtandaoni, ama yakakukuta hayo mengineyo.

Kuepuka usumbufu, na kama hela yako ni ya Manati kama yangu, ni bora kuwatumia ma Agents wa huko ulipo vile utakuwa unadeal nao face to face na sio mambo ya simu na emails. Au kama una mtu unafahamiana naye huko unapotaka kuagiza, then changua online yeye akuhakikishie kama ipo kabla hujaanza process za malipo.

Au achana na kununua Gari, panda 'Bajaji' na 'Daladala' kama mimi. (Joke)


Wenye uzoefu zaidi watakusaidia/watakushauri.


 
YAANI HAMSIKI NDUGU ZANGU HAYA MAKAMPUNI NI BEST KINOMA

http://www.cartechjapan.com/search.asp
www.beforward.com
www.rao-international.COM
www.tradecarview.com hawa watangazaji


TRA
CIF*5%= A
A*20%=B
B*20%=C

A= JIBU LA KWANZA
A= JIBU LA KWANZA UNAZIDISHA NA 20 ASILIMIA
C=JIBU LA PILI UNAZIDISHA NA ASILIMIA 20

SAWA NI BEI UTAKAYOPIGWA TRA HAYO MAGARI CHINI YA CC 2000
UKIWA NA EXAMPTION UNALIPIA ASILIMIA 20 TU

Kuna ki-site hiki hapa mimi kinanisaidia ku-kokotoa kodi utakayolipa kwa TRA fasta:

http://www.gariyangu.com/

Ila nimewauliza wataalamu wangu kwenye thread nyingine waihakiki, lakini bado hawajatoa majibu kama hiyo site ipo sahihi kabisa ama la. Ila kwa baadhi ya cases walizozitoa huko nyuma inaonekana iko sahihi.
 
Back
Top Bottom