Nataka kuandika Wosia

Nataka kuandika Wosia

Mamndenyi

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
43,242
Reaction score
60,939
Salamu sana wanabodi wote,

Mi ni mama nina watoto wanne, mmoja kati yao ni msichana.

Kabla ya maisha haya nilikuwa kwenye ndoa ambayo tumetengana tena bila talaka kwa miaka zaidi ya kumi sana.

Ninaomba ushauri kuhusu hili

- Nataka niandike wosia kuwa vitu vyote nilivyonavyo (yaani nilivyotafuta baada ya kutengana) ni mali ya binti, ila awaangalie kaka zake.

Sababu kubwa ya kuwaza hivi ni kuwa baba yao ana mali pia zikiwepo tulizotafuta naye, na kwa mila za kwao
mtoto wa kike hawezi kuambulia kitu kutoka kwa baba yake.

Naomba ushauri wenu.
Wale watani zangu hapa niko siriaz ukiona ushauri wako utaniumiza, pita tu kimya kimya,
 
Amani ya bwana itushukie wote.unahitaji matibabu ya saikoloji nionavyo mimi bado unaguswa tukio la kuachana na babayao wote ni watoto wako kuwa kwao wanaume hawajapanga na babayao ukikumbuka watoto wako nawao wakiume wamo kwa namna yoyote ile.
 
Huyo mume wako uko aliko ameona na ana watoto wengine?

1. Je huyo mke wake (kama anaye) na yeye mwenyewe (Ex-Mmeo) anawajali hao watoto wenu?

2. Nani anaishi na hao watoto wanne mlionao?

3. Mila zipo na sheria zipo, je unauhakika hizo mali za mmeo zitagawanywa kwa kufata Mila ama na yeye alishaandika Wosia?

4. Wosia wa Mumeo (kama upo) umeshawahi kuuona?
 
1. Ameoa na ana watoto.
2. Pengine watoto wanajua kama wanapewa chochote, kwani sasa ni wakubwa.
3. Watoto niko nao.
4. Hii ya kugawanya mali kwa watoto wa kiume niliwahi kushuhudia
5. Sijui kama amewahi andika wosia.

Huyo mume wako uko aliko ameona na ana watoto wengine?

1. Je huyo mke wake (kama anaye) na yeye mwenyewe (Ex-Mmeo) anawajali hao watoto wenu?

2. Nani anaishi na hao watoto wanne mlionao?

3. Mila zipo na sheria zipo, je unauhakika hizo mali za mmeo zitagawanywa kwa kufata Mila ama na yeye alishaandika Wosia?

4. Wosia wa Mumeo (kama upo) umeshawahi kuuona?
 
1. Ameoa na ana watoto.
2. Pengine watoto wanajua kama wanapewa chochote, kwani sasa ni wakubwa.
3. Watoto niko nao.
4. Hii ya kugawanya mali kwa watoto wa kiume niliwahi kushuhudia
5. Sijui kama amewahi andika wosia.
shimbonyi mono wama. ninachojua mie unatakiwa umwone mwanasheria pamoja na watu wawili wako wa karibu then unayasema yote na kuyaweka katika maandishi then mnafunga kwa pamoja hadi cku ile ambayo mimi na wewe hatuijui itakuja lini then hiyo siku ikitokea ndo yatakuja kusomwa uliyoyasema mbele za watu na kama kuna watu wenye Hofu ya Mungu watayazingatia ila kama hakuna wenye hiyo hofu chochote chaweza tokea.
 
Haika mnu,
Asante kwa ushauri wako nimeuona.
shimbonyi mono wama. ninachojua mie unatakiwa umwone mwanasheria pamoja na watu wawili wako wa karibu then unayasema yote na kuyaweka katika maandishi then mnafunga kwa pamoja hadi cku ile ambayo mimi na wewe hatuijui itakuja lini then hiyo siku ikitokea ndo yatakuja kusomwa uliyoyasema mbele za watu na kama kuna watu wenye Hofu ya Mungu watayazingatia ila kama hakuna wenye hiyo hofu chochote chaweza tokea.
 
Mi nafikiri kama urithi wape tu wote usibague, yawezekena hata huyu baba anaweza kuanyima hata hao watoato wa kiume. Nachukia makabila yanayoangalia mila badala ya familia iliyobaki
 
Mi nafikiri kama urithi wape tu wote usibague, yawezekena hata huyu baba anaweza kuanyima hata hao watoato wa kiume. Nachukia makabila yanayoangalia mila badala ya familia iliyobaki

Asante sana kwa ushauri wako.
 
  • Thanks
Reactions: awp
Jamani, kwani hao wa kiume si wanao?
Hata kama ni chumba kimoja, wagawanyishe wote, wewe ni mzazi wao wote wanne equally.

Hao kama wakipata mali za baba yao, basi ni heri yao. Sasa kwa kuwa mila za baba wa watoto wako zinamtenga msichana, na wewe umeamua kuwatenga wavulana?

Utatengeneza tabaka kati ya wanao bure, na undugu huharibiwa sana na mambo ya urithi, acha watoto wajue hizo mali ni zao wote. Anyetaka zaidi akatafute za kwake kwa elimu aliyoipata.
 
Mkuu Mamndenyi,wosia ni haki yako na utaheshimiwa tu pale wewe utakapofariki (Mungu apishie mbali!).Kikubwa ni kuzingatia kitakiwacho na Sheria Ukishafikiri vyema na kuamua,tuwasiliane kwa ajili ya uandishi wa huo Wosia. Lakini,waweza pia kumpa zawadi mwanao hivyo utakavyo kumpa wakati wa uhai wako sasa.

Wasalimie Kibaha huko. Nami nitakwenda mwisho wa juma.
 
TARATIBU ZA KUANDIKA WOSIA
Taratibu za kuandika wosia zinatofautiana kulingana na sheria ya mirathi inayotumika.

1. WOSIA WA MAANDISHI

Wosia huu unashuhudiwa na watu wawili pale ambapo mtoa wosia anajua kusoma au kuandika.

Shuhuda mmoja lazima awe ndugu wa karibu wa mtoa wosia na mwingine ambaye sio ndugu wa karibu.

Wosia na unatakiwa uwe na tarehe, uandikwe kwa karamu ya wino au upigwe chapa na uwe na saini ya mtoa wosia na saini za mashuhuda ambapo wote wanatakiwa kutia saini zao kwa wakati mmoja.

Mtoa wosia asiye jua kusoma au kuandika awe na mashuhuda wanne wanaojua kusoma na kuandika,muhusia huyo aweke alama ya kidole gumba cha mkono wake wa kulia,mashuhuda hao wote washuhudie na waweke saini zao kwenye Wosia kwa wakati mmoja.

2. WOSIA WA MDOMO/MATAMSHI

Wosia huu unashuhudiwa na mashuhuda wasiopungua wa nne wawili kati yao ndugu wa mtoa wosia na wawili waliobaki wasio ndugu wa mtoa wosia.Wosia huu utolewa na mtu asiye jua kusoma na kuandika.

TARATIBU ZA KUANDIKA WOSIA KATIKA SHERIA ZA MIRATHI

Wosia katika Sheria za kimila,zipo katika jedwali la 3 la Sheria ya (The Local Customary Law (Declaration|) No. 4 Order,1963.

Wosia katika Sheria za kiserikali,zipo katika sheria iliyorithiwa kutoka kwa Waingereza ya(The Indian Succession Act ),iliyopitishwa huko India mwaka 1865.

Hauna tofauti kubwa na wosia wa kimila isipokuwa wosia huu unatakiwa uwe katika maandishi.Vipengele vyote vya wosia wa maandishi vinatumika.

Mtoa wosia anaweza kufuta au kuongeza maneno mengine kwa kuandika maandishi mengine ambayo yatatakiwa kuzingatia masharti ya uandikaji wosia.

Wosia katika Sheria za kiislamu, mtoa wosia anaruhusiwa kuuusia 1/3 ya mali yake 2/3 lazima irithiwe na warithi halali.

UMUHIMU WA KUANDIKA WOSIA

Unaweka mambo bayana kuondoa utata kwa familia na jamaa zako.
Unamchagua msimamizi wa mirathi unayemtaka wewe.
Unatoa maelezo ya wapi mwili wako uhifadhiwe, taratibu zitakazotumika kuuzika mwili wako na jinsi gani mali yako igawanywe kama upendavyo wewe na kwa mujibu wa Sheria.

MASHARTI YA WOSIA

Mtoa wosia lazima awe na akili timamu.

Awe ametimiza miaka kumi na nane (18) na kuendelea.

Uonyeshe tarehe,mwezi na mwaka ulioandikwa.

Uonyeshe majina ya warithi.

Mtoa wosia ahusishe mali zake binafsi na si za mtu mwingine.

Wosia ni siri wanufaika hawatakiwi kuujua.

Ushuhudiwe na mashaidi wawili, kwa mtoa wosia anaye jua kusoma na kuandika na kwa yule asiye jua kusoma ua kuandika mashuhuda wake lazima wawe wanne na wajue kusoma na kuandika.

Mtoa wosia lazima aweke saini yake,na kama hajui kusoma na kuandiaka aweke alama ya dole gumba la mkono wa kulia.

Mashuhuda lazima waweke saini zao tena kwa wakati mmoja.

SABABU ZINAZOWEZA KUSABABISHA MTOA WOSIA KUTOMRITHISHA MRITHI WAKE

Kumtelekeza mtoa wosia pale ambapo anaumwa na kuhitaji msaada.

Kufanya uzinzi na mke wa mtoa wosia.

Endapo kifo cha mtoa wosia kitakuwa kimesababishwa na mrithi.
 
Ngoja kina lissu waje utasaidiwa tu Mamndenyi kumbe uliolewa uchagani?aisee kule ke arithi hata siku moja ni vema ujipange kwa faida ya wanao wote!
 
Last edited by a moderator:
Sasa mamamkwe tuongee dili,ndiowaanza nimeajiriwa huyo bint hanifaikweli menikaweka ndani?ni pm tafadhari
 
Back
Top Bottom