Nataka kuandika Wosia

Nataka kuandika Wosia

Asante nazidi kupata mawazo mazuri juu ya kuandaa hicho kitu,
kwa mfano, nyumba niliyojenga nikiwa kwenye ndoa na ambayo kwa
hii miaka mingi anaishi mwanaume na watoto wake aliozaa na wamama
wengine, je naweza nayo kuiandika kwenye wosia wangu,
ila iwe ni kwa watoto wangu tu?

Lakn la kuzingatia hpo n kwamba wosia unapotolewa na mtu ni lazima ile mali n ya kwakwe binafsi anayotaka kutoa ila kama sio yake binafsi hawez kutoa mfano kama hyo nyumba yenu ni ya ndoa hvo ama mkubaliane na baba yao au kuwe na talaka itakayowafanya mtengane kisheria ili ile mali mgawane alafu yako ndo uandike wosia kumpa mtakaye kwasababu tayar n yako binafsi.
Ila Mungu anachukia talaka sijapenda kukushaur kutaka talaka
 
Lakn la kuzingatia hpo n kwamba wosia unapotolewa na mtu ni lazima ile mali n ya kwakwe binafsi anayotaka kutoa ila kama sio yake binafsi hawez kutoa mfano kama hyo nyumba yenu ni ya ndoa hvo ama mkubaliane na baba yao au kuwe na talaka itakayowafanya mtengane kisheria ili ile mali mgawane alafu yako ndo uandike wosia kumpa mtakaye kwasababu tayar n yako binafsi.
Ila Mungu anachukia talaka sijapenda kukushaur kutaka talaka


Ushauri utazingatiwa.
 
Nilifaidi namna ya kuandika usia kiasi. kama naweza kupata fomat yake maana babu amenipa shamba ila hatujaandikisha. msaada jamani
 
Sasa Mamndenyi huyu mtu unaenda kumuhudumia Mungu akubariki kwa kuonyesha nia ila kama yule mke wake yupo usiende. Tuma hela.
 
salam wana jukwaa
Nataka kuandika wosia lakini sijui nianzie wapi na nifanye vipi. naomba muongozo wa kuandika wosia huo.
Nawasilisha tafadhali
 
salam wana jukwaa
Nataka kuandika wosia lakini sijui nianzie wapi na nifanye vipi. naomba muongozo wa kuandika wosia huo.
Nawasilisha tafadhali
nahoza vipi una miaka mingapi au unataka desa ya mwanafunzi umetumia ujanja!
 
TARATIBU ZA KUANDIKA WOSIA
Taratibu za kuandika wosia zinatofautiana kulingana na sheria ya mirathi inayotumika.

1. WOSIA WA MAANDISHI

Wosia huu unashuhudiwa na watu wawili pale ambapo mtoa wosia anajua kusoma au kuandika.

Shuhuda mmoja lazima awe ndugu wa karibu wa mtoa wosia na mwingine ambaye sio ndugu wa karibu.

Wosia na unatakiwa uwe na tarehe, uandikwe kwa karamu ya wino au upigwe chapa na uwe na saini ya mtoa wosia na saini za mashuhuda ambapo wote wanatakiwa kutia saini zao kwa wakati mmoja.

Mtoa wosia asiye jua kusoma au kuandika awe na mashuhuda wanne wanaojua kusoma na kuandika,muhusia huyo aweke alama ya kidole gumba cha mkono wake wa kulia,mashuhuda hao wote washuhudie na waweke saini zao kwenye Wosia kwa wakati mmoja.

2. WOSIA WA MDOMO/MATAMSHI

Wosia huu unashuhudiwa na mashuhuda wasiopungua wa nne wawili kati yao ndugu wa mtoa wosia na wawili waliobaki wasio ndugu wa mtoa wosia.Wosia huu utolewa na mtu asiye jua kusoma na kuandika.

TARATIBU ZA KUANDIKA WOSIA KATIKA SHERIA ZA MIRATHI

Wosia katika Sheria za kimila,zipo katika jedwali la 3 la Sheria ya (The Local Customary Law (Declaration|) No. 4 Order,1963.

Wosia katika Sheria za kiserikali,zipo katika sheria iliyorithiwa kutoka kwa Waingereza ya(The Indian Succession Act ),iliyopitishwa huko India mwaka 1865.

Hauna tofauti kubwa na wosia wa kimila isipokuwa wosia huu unatakiwa uwe katika maandishi.Vipengele vyote vya wosia wa maandishi vinatumika.

Mtoa wosia anaweza kufuta au kuongeza maneno mengine kwa kuandika maandishi mengine ambayo yatatakiwa kuzingatia masharti ya uandikaji wosia.

Wosia katika Sheria za kiislamu, mtoa wosia anaruhusiwa kuuusia 1/3 ya mali yake 2/3 lazima irithiwe na warithi halali.

UMUHIMU WA KUANDIKA WOSIA

Unaweka mambo bayana kuondoa utata kwa familia na jamaa zako.
Unamchagua msimamizi wa mirathi unayemtaka wewe.
Unatoa maelezo ya wapi mwili wako uhifadhiwe, taratibu zitakazotumika kuuzika mwili wako na jinsi gani mali yako igawanywe kama upendavyo wewe na kwa mujibu wa Sheria.

MASHARTI YA WOSIA

Mtoa wosia lazima awe na akili timamu.

Awe ametimiza miaka kumi na nane (18) na kuendelea.

Uonyeshe tarehe,mwezi na mwaka ulioandikwa.

Uonyeshe majina ya warithi.

Mtoa wosia ahusishe mali zake binafsi na si za mtu mwingine.

Wosia ni siri wanufaika hawatakiwi kuujua.

Ushuhudiwe na mashaidi wawili, kwa mtoa wosia anaye jua kusoma na kuandika na kwa yule asiye jua kusoma ua kuandika mashuhuda wake lazima wawe wanne na wajue kusoma na kuandika.

Mtoa wosia lazima aweke saini yake,na kama hajui kusoma na kuandiaka aweke alama ya dole gumba la mkono wa kulia.

Mashuhuda lazima waweke saini zao tena kwa wakati mmoja.

SABABU ZINAZOWEZA KUSABABISHA MTOA WOSIA KUTOMRITHISHA MRITHI WAKE

Kumtelekeza mtoa wosia pale ambapo anaumwa na kuhitaji msaada.

Kufanya uzinzi na mke wa mtoa wosia.

Endapo kifo cha mtoa wosia kitakuwa kimesababishwa na mrithi.
Shukrani kwa andiko zuuri... But huu sio utaratibu wa kuandika wosia...

Bali umeelezea tu jinsi ya kuandaa wosia.

Ninachohitaji kujua ni zile steps... Yaani naanzia kwa mwenyekiti wa mtaa... Naenda mahakamani... Labda sijui naenda bomani...

Km nimeoa lazima niwe na mke wangu kwenye kutia saini ama....


Yaani flow zile steps zoote hadi wosia unaukamata mkononi
 
Mama angu kwema ulifanikiwa? Usije ukawatoa watoto zako kwenye kurithi pasipo sababu za msingi... Kila anayestahili kupata haki yake na apate
 
Back
Top Bottom