1.Passion.
2.Knowledge
3.Capital pesa
4. Ardhi yenye rutuba
5.Mbegu.
6.Hali ya hewa inayokubali maharage, ni joto la kadri.
7.Mbegu zinazopendwa kwa ukanda wako, mbeya kipapi na njano, mwasipenjele., njombe njano kijani
8. Msimu wa kupanda ni wa mvua na kiangazi.
9. Msimu wa mvua ni disemba na march.Wengi hupanda march kukwepa mvua haribufu.
10.Msimu wa mvua ni muhimu kupiga madawa ya ukungu.
11.Msimu wa kiangazi hulimwa kwenye mabonde oevu au kando ya vyanzo vya maji ili kumwagilia.
12.Mbolea ni za samadi na kisasa.
14. Szmadi ni junia za debe kumi walau 5, ya kuku ni nzuri zaidi,ya ng'mbe ina otesha nyasi na wadudu wahatibifu, kama sio muisilamu ya nguruwe nayo hutumika na ina nguvu sana.
15.Ya dukani mfuko mmoja miksa dap na can. Vilevile itategemea na ardhi ya huko.
Ardhi nzuri mbolea hazitumiki kabisa(virgin land).
16.Mbegu kwa heka debe 1.5 mpaka 2 inategemea na ukubwa wa maharage.
17.Palizi: Inategemeana na msimu na unakolima, Njombe hawafanyi palizi iwapo utapanda march, Mbeya palizi ni lazima mara moja tu.
18.Inakidiriwa katika hali nzuri utavuna debe 32 kwa heka moja.
Sawa na junia 3 za debe 10.
Bei ya kuuza inategemea mahala ulipo be msimu wa kuuza.
Msimu mzuri wa kiangazi debe hufika mpaka 35000 na wa mavuno ni 23000 au 25elf .
Mwaka jana nimenunua mbegu debe 45000 kipapi ya mbeya.
Songea bei huwa mpaka sh 700 kwa kilo msimu wa kununua.
Changamoyobni nyingi ila kubwa kuwwaweka wati wskudimamie shamba.
Binafsi nimeingia hasara mwaka huu.nilitmia kanuni zote za kupanda ila msimamizi aliunguza maharage kwa sumu iliozidi.
Picha hizi hapa.
View attachment 1782264View attachment 1782264
Walifanya uzembe hawakupalilia. Hivyo kuna magugu yaliothiri hapo.
Nililima kwa dhumuni la kupata mbegu kwa ajili ya kulima heka 10 mwakani , basubiri nione ntapata debe ngapi ila 32 ni ngumu japo yaliota vizuri sana na ardhi ina rutuba sana.Nilitumia laki 300000 kwa heka.
Best wish.