Nataka kuanza kujipikia, je napikaje wali kwenye rice cooker?

Nataka kuanza kujipikia, je napikaje wali kwenye rice cooker?

Habari ya wakati huu wakuu.

Kwa muda mrefu sana sijawahi kupika, sasa nataka nianze kujipikia simple foods napokua nyumbani.

Sasa niliwahi kununua hii kitu inaitwa rice cooker ya kilo 2 muda mrefu sana ila kwa kua hua sipiki hivyo sijawahi kujua naipikiaje.

Ningependa kujua kama nataka kupika nusu kilo naweka maji kiasi gani? Nisije kupika ikawa uji, maana juzi nilipika kwa sufuria kwenye gesi ikawa kituko.

Naomba pia mnifundishe simple foods za kupika nyumbani, nimechoka kula kula migahawani.

Najua kuchemsha supu ya kuku wa kienyeji, kuchemsha chai, kupika ugali, kupika nyama. Natamani kujua zaidi.

Ahsanteni.

Kwa kutumia RICE COOKER kipimo cha mchele ndiyo kipimo hichohicho cha maji.

Mfano ukiweka kikombe kimoja cha mchele, weka vikombe viwili vya maji, chumvi wastani na mafuta kidogo. Hapo unakuwa umemaliza, subiria kiive tu.
 
Dahh,majibu ya hapa ni kichefuchefu.
Anyway,mkuu osha mchele wako vema,pima maji kutegemeana na kiasi kilichoelekezwa,weka mchele ndani ya rice cooker yako wakati tayari ukiwa umesha weka chumvi na mafuta,kisha weka kwenye umeme.
Kumbuka hapo kwenye rice cooker kuna taa za rangi mbili au tatu kutegemea na aina ya rice cooker,ile tas nyekundu ndio kiashiria kwamba rice cooker yako yako inafanya kazi,kisha itawaka ya kijani/njano na hiyo tafsiri yake ni kwamba kitu kimeiva so ni wewe kucheki tu kama umekauka kiasi upendacho then pakua piga mlo kwa raha zako.

Ushauri safi kabisa.

Majibu mengine humu ni ukakasi kweli kweli.
 
Chukua kitunguu weka kwenye maji changanya na chunvi ya kutosha ...
Pia nyanya ni muhimu sana ili rice cooker iivishe wali vizuri.
Weka wali wako baada ya kuweka nyanya na vitunguu....kisha jaza maji hadi juu ...angalia maji yasifulumie
Siyo kila Jukwaa ni Chitchat, kawaida ya hili Jukwaa hakunaga majibu ya hovyo hovyo kama haya.
Kama hujui kaa kimya kama wengine.
Weka mchele,changanya na sukari vijiko sita chumvi nusu kijiko,mafuta kikombe cha rice cooker kimoja,katia ndimu mbili. Weka maji kiasi yafunike mchele halafu chomeka kwenye soket uiwashe.
 
Duuh mkuu upo mwenyewe umenunua rice cooker la kilo2??
 
Wakati nephews wangu wanakwenda university ni niliwafundisha kijiji ki kubwa cha chakula mafuta, 1/2 kijiko cha chai chumvi, kikombe kimoja mchele, vikombe viwili maji na moto mdogo hapo lazima wali utoke kwenye sufuria ya kawaida.
 
Back
Top Bottom