Nataka kuanza kujipikia, je napikaje wali kwenye rice cooker?

Kama hapo hakuna majirani, google mkuu hapa utapika wali una mchuzi.
 
Rice cooker haipiki usiku, jitahidi kuiwasha mchana kweupe ili zile taa zake zisijekuonyesha hatari yeyote kwamaana mchele au unga vyote ni sawa tu katika umeme.

Ni hayo tu!
 
Jamani we chenge hujui kupika
 

Kwa kutumia RICE COOKER kipimo cha mchele ndiyo kipimo hichohicho cha maji.

Mfano ukiweka kikombe kimoja cha mchele, weka vikombe viwili vya maji, chumvi wastani na mafuta kidogo. Hapo unakuwa umemaliza, subiria kiive tu.
 

Ushauri safi kabisa.

Majibu mengine humu ni ukakasi kweli kweli.
 
Chukua kitunguu weka kwenye maji changanya na chunvi ya kutosha ...
Pia nyanya ni muhimu sana ili rice cooker iivishe wali vizuri.
Weka wali wako baada ya kuweka nyanya na vitunguu....kisha jaza maji hadi juu ...angalia maji yasifulumie
Siyo kila Jukwaa ni Chitchat, kawaida ya hili Jukwaa hakunaga majibu ya hovyo hovyo kama haya.
Kama hujui kaa kimya kama wengine.
Weka mchele,changanya na sukari vijiko sita chumvi nusu kijiko,mafuta kikombe cha rice cooker kimoja,katia ndimu mbili. Weka maji kiasi yafunike mchele halafu chomeka kwenye soket uiwashe.
 
Duuh mkuu upo mwenyewe umenunua rice cooker la kilo2??
 
Wakati nephews wangu wanakwenda university ni niliwafundisha kijiji ki kubwa cha chakula mafuta, 1/2 kijiko cha chai chumvi, kikombe kimoja mchele, vikombe viwili maji na moto mdogo hapo lazima wali utoke kwenye sufuria ya kawaida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…