Nataka kuanza kusoma masomo ya sekondari kupitia elimu ya watu wazima

Nakupa moyo, kasome. Tena soma kadri utakavyoweza.

Elimu haina mwisho, na kadri unavyosoma unapanuka mawazo kwa namna nyingi sana.

Ukiwa na maswali zaidi kuwa huru kuniuliza, mm ni mwalimu wa QT na resitters, nafundisha masomo yote ya arts.

MUNGU akusimamie na akusaidie katika malengo yako.
 
Amina
 
Zikipungua pumba zangu,zinabaki za kwako uliyesoma .. na ndizo hizi ulizozimwaga hapa.
Shukran
Usikasirike mkuu, hapa jf Kuna watu wengine wapo kwa ajili ya kukatisha tamaa wenzao
 
Mimi nilikuwa na tatizo linalokaribiana na lako kwa asilimia 52.
Nikasoma, nikakaza buti na hatimaye nikafanikiwa.

Kiujumla ni kazi kubwa mno kufaulu mtihani kwa watahiniwa wa kujitgemea, ila ukijitoa kikweli kweli lazima ufaulu.

Kwa mbinu nilizotumia mimi, nikafanikiwa kwa ufaulu mzuri, nikiona mtu ana nia kama yako ninashauku ya kumsaidia kimawazo ili naye afanikiwe.

Hii ni kwa kuwa ukileta jitihada kama zile za wanafunzi wa kawaida, kufeli inakuhusu. Laa sivyo jitihada ziwe mara dufu zaidi ya hivyo.

N.B. Fanya utafiti mdogo kwa kuangalia matokeo ya watahiniwa wa kujitegemea kwa kutazama kiwango chao cha ufaulu. Utagundua ufaulu wao ni mdogo sana. Hapo utagundua kuwa kuna sababu kuu tano zinazosababisha hali hii.

Nikirudi nitazieleza.

ITAENDELEA......
 
Nakusubiri mkuu urudi ili uelezee
 
Elimu haina mwisho.
Muhammad s.a.w.
Mtume WA waislam anasema "ifate elimu hata china"
 
Kila la kheri.
Binafsi nashauri ufanye kozi ya kitu unachotarajia kukifanya baadae.
 
Kama unasoma ukidhank shule itakusaidia kupata pesa, usisome mkuu ila kwa ajili ya kujiongezea maarifa soma tu, elimu ni chachu ya mafanikio ila kwa umri wako bora utumie muda wako kutafuta elimu ya biashara, ujasiriamali ambayo huhitaji cheti bali maarifa msingi.
 
Elimu ya ujasiriamali ninayo tayari na ninaifanyia kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…