Nataka Kuanzisha Bendi ya Muziki

Nataka Kuanzisha Bendi ya Muziki

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2007
Posts
23,265
Reaction score
17,120
Wakuu,
Nilipokuwa likizo nilifurahia sana burdani ya muziki wa bendi. Sasa nafikiria kuanzisha yangu kama uwekezaji fulani.Nkaraibisha maoni yenu kama hii bizinesi ni ya ukweli au la.Pia naomba ushauri wa kitaalamu kuhusu vyombo,ufundi na usimamizi wake.
Shukran Awal....
 
Mkuu unasema ulifurahia muziki wa bendi zipi, za zamani (msondo, sikinde) au za kisasa (twanga pepeta0?
 
naomba utakapoanzisha....katika safu ya masteji shoo...count on me
 
Kabla ya kuanzisha nakushauri umuone Mudhihir,Kapuya,Komba,Banza,Choki,Kasyanju,Muumin,Lady Jay Dee... Hawa wana uzoefu wa bendi...
 
Wasiliana na hawa watu:-

Asha Baraka(Twanga Pepeta)
Juma Kapuya (AKUDO)
Mshoro (Rufita Connection)
 
Kabla ya kuanzisha nakushauri umuone Mudhihir,Kapuya,Komba,Banza,Choki,Kasyanju,Muumin,Lady Jay Dee... Hawa wana uzoefu wa bendi...

Shida sio members humu...halafu kwa vile mimi ntakuwa mshindani wao watanipa ushauri mbovu kama vile kuroga,kuuwa mazeruzeru nk...sitaki hayo...
 
Wakuu,
Nilipokuwa likizo nilifurahia sana burdani ya muziki wa bendi. Sasa nafikiria kuanzisha yangu kama uwekezaji fulani.Nkaraibisha maoni yenu kama hii bizinesi ni ya ukweli au la.Pia naomba ushauri wa kitaalamu kuhusu vyombo,ufundi na usimamizi wake.
Shukran Awal....

Wasiliana na mimi nina bendi ya kwaya Kanisani kwangu
 
Utafiti wa mtu mmoja niliye muona pale BASATA anaitwa Ruhala ni kuwa Bendi nyingi hazidumu kwa kuwa wenye bendi hawaanzishi kibiashara bali kwa misukumo binafsi(Kasyanju na Asha) au Siasa(Komba)...hakuna planning mtu anaamua tu kuanzisha bendi...kwa Komba type hakuna taabu kwa kuwa anapata subsidy ya CCM...hao wengine wanakuwa waninject capital everynow and then bila kufanya ROI(Return On Investment) analysis.

Sababu nyingine ni kuwa bendi ianpohamahama kumbi vyombo huchakaa sana na hivo kufupisha uhai wake.Huko vakesheni nilikokuwa vyombo havimilikiwi na mwenye bendi bali humilikiwa na mwenye ukumbi. bendi inakuja tu kutumbuiza na kuondoka na ndio naona hii ni viable zaidi.
 
AKHA...Nyiye wachungaji mwaijua pesa kwelikweli...tutatoana roho tu

Nina kuhahakikishia utabarikiwa wewe na Kizazi chako chote! Maana kanisa likiwa na band basi ujue neno litaingia waumini na kondoo wengi hawatapotea
 
naomba utakapoanzisha....katika safu ya masteji shoo...count on me

Preta utaweza hii kazi kweli?

090618-09-hip-hop-band-on-stage.jpg
 
Back
Top Bottom